Na Jicho la mdadisi blog, Musoma.
Mahakama Ya Wilaya Ya Musoma Imewahukumu Vijana Watano Kwenda Jela Miaka Sitini Kwa Kila Mmoja Baada Ya Kupatikana Na Hatia Ya Unyanga'anyi Wa Silaha.
Mbali Na Kifungo Hicho Lakini Pia Watu Hao Watalazimika Kulipa Fidia Ya Baiskeli Yenye Thamani Ya Shilingi Laki Nne Kwa Mlalamikaji Ikiwa Ni Pamoja Na Kupewa Adhabu Ya Viboko 24 Kila Mmoja.
Hukumu Hiyo Imetolewa Siku Ya Jumatano Na Hakimu Wa Wilaya Ya Musoma Bw. Richard Maganga, Mbele Ya Waendesha Mashitaka Wa Serikali Bw. Stephano Mgaya Na Jonsi Kaijage.
Waendesha Mashtaka Hao Waliielezea Mahakama Hiyo Kuwa Watuhumiwa Walitenda Kosa Hilo Terehe 27 Mwezi Machi Mwaka Huu Baada Ya Kumvamia Na Kumjeruhi Bw. Fredirick Aloyce Mkazi Wa Kigera Na Kisha Kumkata Kata Na Mapanga Sehemu Mbalimbali Za Mwili Wake.
Vijana Hao Ambao Wamehukumiwa Miaka Sitini Kwa Kila Mmoja Ni Pamoja Na Godrey Mganga, Nyambaryanyambarya, Ramadhani Ismail, Babu G Mafuru Na Hamis Jafari Wote Wakiwa Ni Wakazi Wa Kata Za Kamnyonge Na Nyamatare.
No comments:
Post a Comment