HABARI ZA KIMATAIFA

KENYA YAPATA PIGO.. WATANO WAMEUAWA

Polisi kenya wakiwa katika kuimarisha ulinzi

Watu watano wameuwawa na wengi kujeruhiwa kwenye shambulio katika kituo cha basi mjini Nairobi, Kenya

Inaarifiwa kuwa maguruneti kama mane yalirushwa kutoka kwenye gari dhidi ya kituo cha basi mjini Nairobi - kituo cha Machakos Bus Station, ambacho kilikuwa kimejaa wateja.

Shambulio hilo limetokea Jumamosi saa mbili usiku.

Hadi sasa inajulikana kuwa watu watano wamekufa, na wengi kujeruhiwa.

Mbunge wa jimbo hilo la Kamukunji, Yusuf Hassan, alisema alihisabu majeruhi 40 walipokuwa wakifikishwa hospitali ya taifa, ya Kenyatta.

Wakuu bado hawakueleza nani alihusika na shambulio hilo; wala kama washambuliaji ni wa ndani au kutoka nje ya nchi.

BBC - swahili


>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>


Jeshi la Taifa la Cyrenaica, utawala mpya wa Benghazi nchini Libya (reuters)
BENGHAZI

Viongozi wa wapiganaji na wa makabila katika mji wa Benghazi nchini Libya wamejitangazia utawala wao katika eneo la mashariki mwa nchi kama jimbo lenye uhuru.
Wanasema wanarejea makubaliano ya tangu miaka ya 1950 ya jimbo hilo, likijulikana kama Cyrenaica, lilivyoendeshwa kwa asilimia kubwa ya utawala.
Wengi wa watu wa Benghazi wamekuwa wakilalamika kuachwa nyuma na kubaguliwa kwa jimbo lao ambalo lina utajiri mkubwa wa mafuta Hatua hiyo inaleta wasiwasi kwa utawala wa muda mjini Tripoli

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>

TRIPOL


Umati wa watu umeingia mitaani kushangilia kile kinachoonekana mwisho wa utawala wa kiongozi wa nchi hiyo Kanali Muhammar Gaddafi, baada ya waasi kuingia katika mji mkuu wa nchi hiyo Tripoli.Hata hivyo serikali imedhamiria kupambana na waasi hao.

Msemaji wa waasi hao aliyejitambulisha katika kituo cha television cha Al Jazzera kuwa anaitwa Nasser amesema kuwa vikosi vya serikali vinadhibiti asilimia kati ya 15 na 20 ya mji huo wa Tripoli.

Mapema hii leo waasi wamepeperusha bendera yao huku wakielekea katika eneo la uwanja wa kijani mjini Tripoli, eneo ambalo wameliita eneo hilo kuwa ni uwanja wa mashahidi.

Wakati huo huo Rais Barack Obama wa Marekani amemtaka Kanali Gaddafi kutambua kuwa utawala wake umefikia kikomo na kusisitiza umuhimu wa kipindi cha mpito kuelekea demokrasia kwa amani.

Kwa upande mwingine Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Thomas de Maiziere ameelezea uwezekeno wa kupelekwa kwa vikosi vya Ujerumani nchinim Libya pale utawala wa Kanali Kaddafi utakapoondolewa.

Hadi kufikia hii leo jioni waasi hao wamedai kuudhibiti mji mkuu kwa zaidi ya asilimia 95.


NEW YORK

Baraza la Haki za Binaadamu la Umoja wa Mataifa linakaa leo katika kikao cha dharura hii leo kujadiliana juu ya hali nchini Syria.

Kikao hicho kinakuja baada ya wachunguzi wa umoja huo kupata ushahidi juu ya vitendo vya uhalifu dhidi ya binaadamu vilivyofanywa na vikosi vya serikali ya Rais Bashar al-Assad.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa vikosi hivyo vya serikali ya Syria vimewaua watu elfu mbili katika kipindi cha miezi mitano ya uasi dhidi ya utawala wa miaka 11 wa Rais Assad.

Wakati huo huo wanaharakati wa upinzani nchini Syria wanaingia katika siku ya tatu ya mazungumzo juu ya muundo wa baraza la kitaifa litakaloratibu mapambano dhidi ya serikali.

Hapo jana katika hotuba yake kwa taifa katika televisheni ya taifa, Rais Assad alisema anatarajia uchaguzi wa bunge utafanyika February mwakani.Ameongeza kuwa makundi ya kisiasa mbali ya chama chake cha Baath yataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.


JERUSALEEM

Msemaji wa jeshi la Israel amesema wapalestina mapema leo wamevurumisha makombora matano kuelekea Israel, na kwa upande wao jeshi la anga la Israel limefanya shambulio moja kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Kuibuka kwa mapigano hayo kulikuwa ni mfululizo wa matukio ya kutupiana risasi Alhamisi iliyopita wakati waisraeli wanane walipouawa na kusababisha mashambulio ya kulipiza kisasi.

Polisi watano wa Misri waliuawa wakati wanajeshi wa Israel walipokuwa wakiwasaka washambuliaji wakipalestina na kusababisha mparaganyiko wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barack alielezea kusikitishwa kwake na matukio hayo, lakini Misri ilisema kuwa tamko hilo halitoshi wakati ambapo bado hakuna taarifa zozote za madhara kutoka pande zote katika siku ya tano ya mapigano.

Tayari baadhi za nchi zimeanza kuvunja uhusiano wa kidiplomasia baina yao na nchi ya Israel, Misri imekuwa miongoni mwa nchi za mwanzo kabisa kutangaza nia hiyo.