Saturday, June 8, 2013

KITIMA AAGWA RASMI NA WANAFUNZI WA SAUT MWANZA

HATIMAYE ile sherehe kubwa ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu, leo tarehe 07/06 imeafanyika. Hii ilikuwa ni maalumu kwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) kuweza kuagana na Makamu mkuu wa chuo ambaye amekamilisha kipindi chake cha utumishi , kipindi cha miaka 10, tangu 2003 Dkt Charles Kitima...kwenye picha hii hapa chini yupo upande wa kulia.
Dkt Kitima... anakamilisha utumishi wake huku akijivunia na kuacha kumbukumbu ya ongezeko kubwa la wanafunzi wanaodahiliwa katika chuo hiki kikuu na kikongwe zaidi barani Afrika katika fani ya mawasiliano ya umma, ambapo sasa kina jumla ya wanafunzi 27 elfu, kikiwa na matawi karibu kanda zote hapa nchini.....haya ni baadhi ya matawi ya SAUT... Bukoba, Singida, Tabora, Iringa, Mtwara....haya ni baadhi.
Dkt Kitima anastaafu na nafasi yake itachukuliwa na aliyewahi kuwa makam mkuu wa chuo taaluma, na pia kwa sasa ndie alikuwa makam mkuu wa chuo tawi la Bukoba, Dkt Pius Mgeni.
Picha zote na Elia Migongo, Ahsante kwa Mc Chilwa pia kwa support.
 BURUDANI ZILIFUATA, mara baada ya wimbo wa taifa kuimbwa , wasanii mbali mbal;i walianza kutumbuiza, wa kwanza alikuwa ni MORE MUSIC msanii kutoka SAUT .

 BAADAE MASHAIRI, ilibidi hata kuchuchumaaa....hii ni kutia msisitizo
 BAADA YA MASHAIRI.,,,, kilichofuata ni "kuchikuchi" hapa naikusudia ngoma ya kuchikuchi hotahe...ya kihindi, ila hapa ilichezwa na wanasheria wanafunzi wa SAUT

 BAADAE ..... hotuba , huyu ni president wa wanafunzi wa SAUT MWANZA, akisema yake ya moyoni ...jinsi alivyompenda Dkt Kitima
 BAADHI YA WALIOHUDHURIA 
 BURUDANI TENAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!,.... Kikundi cha ukombozi... hapa ilikuwa ni kusukuma mauno kwa staili za Kiafrika zaidi...na hasa kutoka makabili mbali mbali ya hapa nyumbani Tanzania
Ilibidi msisitizo utolewa ...kwa Lugha ya Kisukuma...hapa ujumbe mkubwa ukawa...ni shukurani kwa Dkt Kitima ...kuvifikisha vijiji vya Luchelele na sweya.... kiuchumi zaidi...maana maeneo haya yamenufaika sanaaa na uwepo wa SAUT na wanafunzi pia


 Ilimbidi Dkt Kitima aseme neno kidogo kwa binti huyu Mwalimu wa mwaka wa Pili,... ambaye wakati Dkt Kitima anafika mwanza ...huyu binti alikuwa shule ya msingi Nyamalango.....sasa Mwakani anahitimu
 HAPA KIJANA wetu Haji Yona aka Mchungaji...akafanya interview na mmoja kati ya wasanii wa Mkombozi....ilikuwa ni sehemu ya matangazo ya moja kwa moja ya kituo cha redio SAUT
 TAFES sasaaaaaaaaaaaaaaaa......sebene lilikuwa kaliiiiiiiiiiiiiii

 UZINDUZI WA KITABU ....hiki kimepewa jina la WARAKA KWA MAFISADI.... waweza fika maktaba ya SAUT mwanza ...ukausoma waraka huo.....Kitabu hiki kimeandikwa na Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza Mawasiliano ya umma.

 HISIA ZA DKT KITIMA ...kwenye hotuba yake
 HAWA NDIO WAZEE WALIOMPOKEA KITIMA MWANZA HIII

 WASHEREHESHAJI WETU......AIDAN na CHILWA 
 ZAWADI SASAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!


 KWENYE INERVIEW   MOJA KWA MOJA REDIO SAUT.... hapa ni dkt Kitima na Mtangazaji wetu ELIA



No comments: