Saturday, June 8, 2013

SIKU YA MAZINGIRA MUSOMA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA
Mwanandish wa blog hii Bw Ahmad Nandonde akizungumza na mkazi wa buhare bima manispaa ya musoma Bw.Magore Mafuru
Wanafunzi wa Buhare wakiadhimisha siku ya mazingira yaliyofanyika dunia nzimaq tareh 5 june
Uongozi Na Wanafunzi Na Wa Chuo Cha Maendeleo Ya Jamii Buhare Kilichopo Katika Manispaa Ya Musoma Mjini Leo Wameadhimisha Siku Ya Mazingira Duniani Kwa Kutoa Elimu Kwa Jamii Inayowazungunguka Ikiwa Ni Pamoja Kuelezea Umuhimu Wa Utunzaji Wa Mazingira.
Hayo Yamesemwa Leo Na Mkufunzi Wa Elimu Chuoni Hapo Bw. Linus Kaindaguza Wakati Akizungumza Na Victoria Fm Walipotembelea Maeneo Yanayozunguka Chuo Hicho.

 Amesema Katika Matembezi Hayo Wameweza Kuwaelezea Madhara Yatokanayo Na Uchimbaji Wa Mashimo Hayo Ambayo Yameweza Kusababisha Maafa Na Hivyo Kuwataka Wananchi Hao Kuanzisha Shughuli Za Kilimo Kama Vile Mboga Mboga Nyanya  Vitunguu Ili Kupunguza Uharibifu Wa Mazingira.
 Aidha Akawaelezea Umuhimu Uchimbaji Wa Vyoo Na Usafishaji Wa Mazingira Ili Kuondokana Na Magonjwa Ya Milipuko Ambayo Ni Hatari Kwa Afya Zao  Huku Akizungumzia Kuwepo Kwa Dampo Lililopo Katika Eneo La Mugaranjabo Ambalo Limekuwa Likiathiri Kwa Kiasi Kikubwa Uharibifu Wa Mazingira
 Awali Akizungumza Kwa Niaba Ya Wakazi Wa Eneo Hilo Bw. Makongo Mafuru Amesema Kuwa Ili Kutatua Tatizo Hilo Ni Wazi Kuwa Serikali Inatakiwa Kuwapatia Mikopo Itakayowawezesha Kujishughulisha Na Miradi Mbali Mbali Kama Vile Ya Ufugaji Ili Kuondokana Na Tatizo Hilo La Uchimbaji Wa Mashimo Hayo.
 Hata Hivyo Hivyo Akailaumu Serikali Kwa Kusema Kuwa Ndiyo Chanzo Kikubwa Chakuwepo Kwa Mashimo Hayo Kwani Walikuwa Wakichimba Mashimo Hayo Kwaajili Ya Kufanikisha Ujenzi Wa Kivuko Kinachoelekea Kinesi Na Bandari Ya Musoma Mjini.
Kwa Upamnde Wake Mwanafunzi Wa Chuo Cha Maendeleo Ya Jamii Bw. Vicent Wana Ameoneshwa Klusikitishwa Kwake Na Kuwepo Kwa Uharibifu Wa Mazingira Ambao Umekuwa Ukifanywa Na Wakazi Wanaozunguka Maeneo Hayo Na Kusema Kuwa Yamekuwa Yakisababisha Madhara Makubwa Mabyo Ni Vifo Hususani Katika Kipindi Cha Mvua Ambapo Mvua Zinaponyesha Husababisha Kujaa Kwa Maji Katika Mashimo Hayo Makubwa Ikiwa Ni Pamoja Kufuga Uhalifu Na Hata Mbu Kuzaliana Na Hivyo Kuathiri Jamii Nzima Kutokana Na Kuugua Ugonjwa Wa Malaria.
 Pia Akawaomba Wakazi Wanaozunguka Eneo Hilo Kushiri Kikamilifu Katika Utunzaji Wa Mazingira Huku Akiwataka Viongozi Wakisiasa Kutoingilia Masuala Ya Kitaalamu  Kwani Suala La Utunzaji Wa Mazingira Ni Suala Ambalo Linalowahusu Watanzania Wote.
 Ili Kuhakikisha  Uchimbaji Wa Kiholela Wa Mashimo Hayo Unatokomezwa Serikali Imeshauriwa Kutoa Elimu Ya Ujasirialmali Kwani Zipo Kazi Nyingi Ambazo Zinaweza Kufanywa Na Wakazi Hao Ili Kuondokana Na Tabia Ya Uharibifu Wa Mazingira.
 Akizungumzia Hayo Huyu Bi Meri Kisamaka Mwanafunzi Wa Chuo Hicho Cha Buhare.
 Hata Hivyo Kwa Upande Wake Afisa Wa Utunzaji Kumbukumbu  Chuoni Hapo Ahmad Hamza Ameoneshwa Kufurahishwa Na Hatua Hiyo Ya Utoaji Elimu Na Kusema Kuwa Suala Hilo Lisiwe Tu Kwa Siku Maalumu Bali Liwe Linafanyika Mara Kwa Mara Ili Kuhakikisha Elimu Ya Utunzaji Wa Mazingira Inawanufaisha Wananchi Na Jamii Kuiujumla.
 Kauli Mbiu Ya Maadhimisho Ya Siku Ya Mzingira Duniani Mwaka Huu Yemebeba Ujumbe Unaosema "Panda Miti Itunze Na Tunza Mazingira"


No comments: