Monday, June 5, 2023

HAKUNA VISA KUINGIA NCHI YA AFRIKA MASHARIKI

Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuondoa gharama ya viza baina yao. Taarifa zaidi zinasema, gharama ya viza imeondolewa kwa watu wanaotaka kusafiri kutoka nchi moja kwenda nyingine ndani ya jumuiya hiyo kwa shughuli mbalimbali zikiwemo za kibiashara. Lengo la uamuzi huo limeelezwa kuwa ni kukuza mahusiano miongoni mwa wakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na kuchochea ukuaji wa biashara na uchumi wa nchi husika. Kuondolewa kwa gharama ya viza ni sehemu ya vikwazo kumi vya kibiashara visivyo vya kiforodha (NTBs) vilivyoondolewa na jumuiya hiyo, huku vikwazo nane vikiendelea kushughulikiwa, na vikwazo vingine vipya vinne vimewasilishwa ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara baina ya nchi hizo. CHANZO#parstoday

No comments: