Tuesday, September 26, 2023
UFARANSA YAKUBALI YAISHE KWA NIGER
Hatimaye, baada ya wiki kadha za vuta nikuvute, Ufaransa imesalimu amri mbele ya
takwa la Niger na kutangaza kwamba, balozi wa Ufaransa nchini Niger, Sylvian
Itte, atarejea Paris katika saa chache zijazo. Tangazo la Ufaransa linasema pia
kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo nao wataondoka Niger ifikapo mwishoni wa mwaka huu.
Sambamba na kutangazwa kwa habari hii, Baraza la Kijeshi la Niger katika taarifa
yake limeeleza kuwa, kuondolewa kwa wanajeshi wa Ufaransa na balozi wa Ufaransa
nchini Niger ni wakati wa kihistoria kwa nchi hiyo na kutangaza katika taarifa
yake kwamba leo tunaadhimisha enzi mpya katika njia ya uhuru na mamlaka ya
kujitawala Niger. CHANZO: PARSTODAY
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment