Monday, June 5, 2023

VURUGU ZAENDELEA NCHINI SENEGAL, HUDUMA YA INTERNET IMEKATWA

Serikali ya Senegal imepunguza ufikiaji wa huduma za intaneti na simu za mkononi katika baadhi ya maeneo kwa sababu ya ghasia mbaya ambapo jumbe za "chuki na uasi" zimetumwa mtandaoni. Nchi hiyo ya Afrika Magharibi imekumbwa na maandamano na ghasia kwa muda wa siku tatu ambapo ambapo watu 16 wameuawa. Ghasia hizo ni mbaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo. Wiki iliyopita, serikali ilizuia upatikanaji wa baadhi majukwaa ya mitandao, lakini watu wengi waliweza kujipenyeza katika mitandao iliyofungwa kwa kutumia mfumo wa VPN ambao huficha eneo la mtumiaji. CHANZO#parstoday

No comments: