Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania jana alikabidhiwa katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba na kuwataka Watanzania waipigie kura za ndio.
Mwenyekiti wa bunge hilo Samuel Sitta alimkabidhi rasmi katiba hiyo Rais Kikwete akiwa pamoja na pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dakta Mohamed Ali Shein kwenye hafla iliyofanyika uwanja wa michezo wa Jamhuri mjini Dodoma.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na pia na viongozi na watu wa matabaka mbalimbali wakiwemo mabalozi wa nchi mbalimbali.
Kikwete alisema kuwa, kazi ya kutunga katiba ilikuwa safari yenye changamoto nyingi.
Baada ya Rais wa Tanzania kukabidhiwa rasimu hiyo, itabakia hatua moja ya kupigiwa kura ya maoni na Watanzania, kazi ambayo haijajulikana bado iwapo itafanyika kabla au baada ya uchaguzi wa mwaka ujao wa 2015.
Sheria iliyopo inataka kura ya maoni kuhusiana na katiba mpya ifanyike katika muda wa siku 84 baada ya rais kukabidhiwa katiba iliyopendekezwa
No comments:
Post a Comment