Thursday, October 9, 2014

WHO: HAKUNA DALILI ZA KUPUNGUA EBOLA

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa hakuna dalili zinazoonesha kuwa kasi ya maambukizo ya ugonjwa wa Ebola inapungua, bali ugonjwa huo unazidi kutishia nchi za Magharibi mwa Afrika ambazo hazina suhula za kutosha za kukabiliana nao.
WHO imesema kuwa, hadi kufikia Oktoba 5 mwaka huu, virusi vya Ebola vimesababisha vifo vya watu 3,879 huku wengine 8,033 wakiambukizwa maradhi hayo ambapo Liberia na Siera Leone zimeathiriwa zaidi na ugonjwa huo. 

Hayo yanajiri huku mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini Marekani akifariki dunia kutokana na maradhi hayo. Thomas Eric Duncan alianza kuugua baada ya kuingia Marekani akitokea Liberia Septemba 20 mwaka huu ambapo baadaye alilazwa hospitalini huko Dallas na kuanza kutibiwa kwa dawa za majaribio.
Haya yamejiri muda mchache baada ya Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani John Kerry kutoa wito kwa nchi zote kuimarisha juhudi zao za kukabiliana na ugonjwa huo.

No comments: