Tuesday, March 18, 2014

WARIOBA AWASILISHA RASIMU YA KATIBA BUNGENI, LICHA YA ZOMEA ZOMEA ZA JANA NA MADAI KUWA MWENYEKITI KAKIUKA KANUNI

Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji Joseph Warioba amewasilisha rasimu ya katiba bungeni mjini Dodoma inayoeleza mapendekezo kadhaa na mapungufu yaliyomo kwenye katiba ya sasa .
Baadhi ya mapendekezo hayo ni pamoja na suala la muungano,huku akionekana kushangiliwa na wajumbe wa bunge hilo jaji Warioba pia amezungumzia suala la taasisi ya urais.
Mapendekezo mengine yaliyomo ndani ya rasimu hiyo iliyowasilishwa na Warioba ni mawaziri na naibu waziri kutokua wabunge,spika wa bunge la jamhuri ya Muungano na naibu wake wasiwe wabunge ili kuepusha upendeleo wa aina yoyote.

Warioba amewasilisha rasimu hiyo baada ya kukamilika kwa utaratibu , ukusanyaji utathmini wa maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya

No comments: