JESHI LA POLISI LAWAFUKUZA KAZI ASKARI WAKE WANNE KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI.....
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya DSM limewafukuza kazi askari Wanne wa jeshi hilo kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya uhalifu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya DSM – SULEIMAN KOVA amewaambia waandishi wa habari uchunguzi wa awali umeonyesha askari hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwa ni pamoja na tukio la ujambazi la Tarehe Tisa mwezi huu katika ofisi ya kampuni ya HONG YANG iliyopo eneo la MBEZI BEACH jijini DSM.
Askari waliofukuzwa kazi ni RAJABU MKWENDA wa Makao Makuu ya Jeshi la polisi, SIMON wa kituo cha Polisi Kati, ALBERNUS KOOSA wa kikosi cha bendi ya polisi DSM na SELEMANI wa kituo cha polisi KIGAMBONI Jijini DSM.
CHANZO TBC
No comments:
Post a Comment