RPC MLOWOLA |
Watu wanne wameuawa alfajiri ya leo katika kata ya BUHONGWA wilaya ya Nyamagana, kitongoji cha IGWAMBITI, watu hao wanasadikiwa kuwa ni wezi wa ng’ombe, ingawa hadi taarifa hizi zikiwa zimemfikia kamanda wa polisi hakuna aliyekuwa ameijtokeza kudai kuibiwa ng’ombe hao.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Valentino Mlowola amewataja watu waliouawa kuwa ni EZEKIEL LUKAS , KUSEKWA LUKAS hawa wote ni ndugu wa familia moja, pamoja na MASUMBUKO KISINZA, hawa watatu walifariki papo hapo.
Mwingine alifariki akiwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando ni MAFISI MWITA yeye alikuwa muuzaji wa nyama katika bucha iliyopo Buhongwa center.
Mauaji hayo yamefanywa na wananchi walioitikia kelele za yowe (MWANO) kutoka kwa kundi la watu waliokuwa wanatokea kata tatu BUHONGWA , MKOLANI, na USAGARA, huku wakiwa na mmoja wa watuhumiwa ambaye inadaiwa ndiye aliyetumika kuwatambua washirika wenzake katika wizi huo,
Bado hata hivyo mtuhumiwa huyo hajapatikana na wala hajulikani alipo baada ya wananchi hao kutoroka nae baada ya polisi kufika eneo la tukio.
Zisikilize sauti za Kamanda Mlowola, na afisa mtendaji wa kata ya Buhongwa.. hapa chini…
SAUTI YA AFISA MTENDAJI WA KATA
SAUTI YA RPC
SAUTI YA AFISA MTENDAJI WA KATA
No comments:
Post a Comment