MUSOMA.NA AHMAD NANDONDE
Kikao cha wanahabari na katibu tawala |
HAYO YAMESEMWA LEO NA KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MCHAN WA LEO KATIKA UKUMBI MDOGO WA MIKUTANO.
OLE KUYAN AMESEMA KUWA MARA BAADA YA IBADA HIYO MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA MPAKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AMBAPO UTAWASILI SAA KUMI NA NUSU ALASIRI KABLA YA KUSAFIRISHWA TENA HADI MJINI DODOMA AMBAPO UNATARAJI KUWASILI SAA KUMI NA MOJA JIONI NA KUHIFADHIWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA.
KWA KUWA ENZI ZA UHAI WAKE MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MJINI DODOMA KAMA MKUU WA WILAYA WANANCHI MKOANI HUMO WATAPATA FURSA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TAREHE 28 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA SITA MCHANA.
BW. OLE KUYAN AMEONGEZA KUWA BAADA YA WAKAZI WA DODOMA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SAA SITA MCHANA MWILI HUO UTASAFIRISHWA TENA HADI KIJIJINI KWAKE KILOSA AMBAPO UTAKABIDHIWA KWA FAMILIA YA MAREHEMU KWAAJILI YA MAOMBOLEZO SAA TISA ALASIRI.
MWILI WA MAREHEMU UTAFANYIWA IBADA IKIWA NI PAMOJA NA WANANCHI WA KILOSA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KWA MARA MWISHO KABLA YA KUPELEKWA KATIKA ENEO LA MAZISHI KWAA JILI YA KUUHIFADHI KATIKA NYUMBA YA MILELE SAA KUIMI NA MOJA JIONI.
MAREHEMU TUPA AMEFARIKI DUNIA JANA WILAYANI TARIME ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NA AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO.
MAREHEMU ALIZALIWA JAN 1 1950.
No comments:
Post a Comment