Wednesday, March 26, 2014

KUELEKEA MIAKA HAMSINI YA TANZANIA, WAKAZI WA BUHARE MUSOMA BADO WANAKABILIWA NA KERO YA MAJI

MUSOMA:
WAKAZI WA MTAA WA MGARANJABO KATA YA BUHARE MANISPAA YA MUSOMA WANAKABILIWA NA TATIZO KUBWA LA UHABA WA MAJI HALI INAYOWALAZIMU KUAMKA SAA NANE ZA USIKU KWENDA KUCHOTA MAJI KWENYE VISIMA VYA CHEMICHEMI AMBAVYO VINATOA MAJI KIDOGO NA KUSABABISHA WAKAZI HAO KUKAA ZAIDI YA MASAA MATATU ILI KUPATA MAJI.
WAKIZUNGUMZA NA VICTORIA FM WAKAZI HAO WAMESEMA KUWA HALI HIYO IMEKUWA KERO KUBWA KWAO KWANI WANATUMIA MUDA MWINGI KUSUBILIA MAJI HALI INAYOPELEKEA KUKWAMISHA SHUGHULI ZINGINE ZA KIMAENDELEO PAMOJA IMEKUWA IKIWAJENGEA MAZINGIRA MAGUMU KWA KUHOFIA USALAMA WAO.
WAKAZI HAO WAMESEMA KUWA TATIZO HILO LIMEDUMU KWA KIPINDI CHA MUDA MREFU NA KUDAI KUWA WALIPOKUWA WAKIONGEA NA VIONGOZI WALIAMBIWA KUWA TATIZO HILO LINASHUGHULIKIWA NA MAJI YATAWAFIKIA MUDA SI MREFU LAKINI MPAKA SASA TATIZO HILO HALIJAPAJIWA UFUMBUZI.
KWA UPANDE WAKE DIWANI WA KATA YA BUHARE BWANA LUCAS KATIKIRO AMEKIRI KUWA SUALA LA MAJI BADO NI TATIZO KUBWA KATIKA KATA HIYO.
KATIKIRO AMEELEZA KUWA TATIZO HILO LINASHUGHULIKIWA KWANI AMESHAANDIKA BARUA MBILI KWA MKURUGEZI WA MUWASA ILI KUOMBA KUPATIWA MAJI KATIKA MTAA HUO AMBAPO ALIMBIWA KUWA TATIZO HILO LINAFANYIWA KAZI KUPITIA MRADI WA MAJI KWANI BAADHI YA MITALO YA MABOMBA YA KUSAMBAZIA MAJI TAYARI IMESHAANZA KUCHIMBWA.
HATA HIVYO DIWANIHUYO AMEWATAKA WANANCHI HAO KUWA WAVUMILIVU NAKUWADHIBITISHIA KUWA HADI SASA AMEKWISHA ANDIKA BARUA YA KUOMBA FEDHA KUTOKA MFUKO WA JIMBO ILI KUWEZA KUCHIMBA VISIMA VIWILI VITAVYOCHIMBWA KATIKA MAENEO YA MCHONGOMANI PAMOJA NA ENEO LA BUHARE BONDENI AMBALO LINALOTENGANISHA KATA YA KIGERA NA KATA YA BUHARE.

No comments: