Tuesday, March 25, 2014

MKUU WA MKOA WA MARA AFARIKI AKIWA KAZINI

JOHN TUPA , Enzi ya uhai wake
Mkuu wa mkoa huo John Gabriel Tupa amefariki hii leo, akiwa kwenye shughuli za kikazi wilayani Tarime akiwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Wilaya ya Tarime kutokana na kupatwa na shinikizo la damu akiwa anapatiwa taarifa ya Wilaya hiyo.
 
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Tawala wa mkoa wa MaraBenedict Ole Kuyan juu ya kifo hicho, imesema mkuu wa mkoa alifika ofisini kwake mapema saa 1 asubuhi na kupeana taratibu za kazi kabla ya kuondoka kwenda wilayani Tarime alikofikwa na umauti akiwa kwenye majukumu ya kazi.

Marehemu alianguka ghfla wakati akipatiwa taarifa mbali mbali za kiutendaji wilayani tarime ambapo baada ya hapo alitakiwa kwenda kufunga mafunzo ya mgambo nyamongo wilayani humo.
Katibu tawala wa mkoa wa mara Benedictor Ole Kuyan kushoto akizungumza na waandishi wa habari mchan wa leo na kulia ni Mkuu wa wilaya ya rorya Bw. Elias Goroi.
askofu akiuombea mwili wa marehemu tuppa baada ya kufikisha katikahospital ya mkoa wa mara.
Wahudumu wa hospital ya mkoa wakiupokea mwili wa mkuu wa mkoa wa mara ukitokea wilayani tarime.
PICHA NA HABARI KWA HISANI YA JICHO LA MDADIS BLOG

No comments: