Thursday, March 20, 2014

SIMON PHILBERT ASHINDA URAIS WA WANAFUNZI SAUT MWANZA

Story ya Nickson Kilunga,Waziri wa habari SAUTSO

Ajizolea kura lukuki
uchaguzi watawaliwa na amani 

Ndugu Saimon Philibert mwanafunzi wa mwaka wa pili kutoka katika kitivo cha sanaa ya elimu (BAED 2) ameibuka kidedea katika uchaguzi wa kumtafuta rais wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino tawi kuu la mwanza baada ya kumshinda mpinzani wake ndugu Godfrey Gaston kutoka kitivo cha sheria (LLB 3)uchaguzi uliofanyika juzi 18/03/2014,Akitangaza matokeo hayo msimamizi mkuu wa uichaguzi huo na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi chuoni hapo bwana Bakari ,alimtangaza ndugu Philibert kuwa mshindi wa nafasi hiyo nyeti kabisa chuoni hapo ambapo Philibert alishinda kwa kura 2582 dhidi ya mpinzani wake ndugu Gaston aliyepata kura 1373 kati ya jumla ya kura 4003 zilizopigwa na kura 8 kuharibika.

Mchakato wa kumtafuta rais wa chuo hicho ulianza tangu tarehe 11/03/2014 kwa wagombea takribani 15 kujitokeza kuchukua form za kuwania urais wa chuo na baada ya mchujo uliofanywa na tume ya

uchaguzi ya chuo yalibakia majina 4 yaliyoongoza miongoni mwa watu hao 15,majina ambayo kiutaratibu hupelekwa ngazi ya juu ya chuo(senet)kwa ajili ya mchujo zaidi na majina mawili kurudi,wagombea walifanya mdahalo mkubwa siku ya jumatatu jioni katika ukumbi wa M13 uliopo chuoni hapo ambapo wagombea walimwaga sera zao na kuulizwa maswali.
akizungumzia uchaguzi huo mmoja ya wajumbe alisema licha ya zoezi zima la uchaguzi kuendeshwa kwa uwazi,haki na huru lakini zilikuwepo changamoto kazaa za wapambe wa wagombea kuchafuana kwa misingi ya vyama na wanafunzi wachache kujitokeza kupiga kura"unaweza kuona chuoni kuna zaidi ya wanafunzi 12500,lakini waliojitokeza kupiga kura ni wanafunzi 4003"hili si jambo jema na halitoi mwelekeo mzuri kwa taifa letu hasa tukitarajia wao kama wasomi kuwa wakwanza kutimiza haki yao hiyo ya kikatiba ili wakawe mabalozi wazuri huko waendapo pindi wamalizapo chuo.
Mgombea mwenza wa Philibert ambaye kwa mujibu wa katiba ya serikali ya wanafunzi anakuwa makamu wa rais ni bi MerryGoreth Gervaz kutoka kitivo cha sayansi ya jamii (BASO 2) na yule wa ndugu Gaston ni bi Barnabas,uchaguzi chuoni hapo hufanyika kila mwaka,na bwana Philibert anakuwa rais wa 11 tangu chuo kianzishwe ambapo anaenda kumpokea kijiti rais aliemaliza mda wake ndugu Dovakamwene Mcheshi.

No comments: