Wednesday, November 27, 2013

UMEME WA TANESCO WALETA SHIDA KWA MITAMBO YA RADIO SAUT

Kumetokea hitilafu ya umeme katika kituo cha kurushia matangazo cha REDIO SAUT FM , majira ya saa kumi jioni leo, kituo hiki kipo eno la "retreat " . Hitilafu hiyo imejitokeza baada ya umeme wa TANESCO kurudi katika hali inayotajwa kuwa ya kawaida baada ya kuwepo kwa mgao wa umeme wa siku takribani 11, ATHARI mitambo yetu ya kuzalishia umeme wa jua imeungua, na hivyo kuathiri piamfumo mwingine wa umeme, MATANGAZO ya kituo hiki kwa sasa hayako hewani , MAFUNDI wetu wanaendelea na juhudi za kurekebisha hali ya mambo mpaka kufikia kesho muda wowote matangazo yatarejea hewani... TUNAOMBA RADHI KWA USUMBUFU ULIOJITOKEZA.
Hili ndilo jengo la mitambo ya kurushia matangazo ya SAUT FM

 Juhudi za kuzima moto zikiendelea
Hii ndio mitambo ya umeme jua ambayo imeungua


No comments: