Friday, November 29, 2013

PICHA 36 ZA COMMUNITY DAY SAUT MWANZA ZIKO HAPA , KAMA HUKUHUDHURIA HII NI FURSA KWAKO

Leo katika chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT)Kampasi kuu ya MWANZA , kumefanyika maonesho ya vitivo mbali mbali vya chuo hicho katika siku maalumu inayojulikana kwa jina la SIKU YA SAUT NA JAMII (SAUT COMMUNITY DAY).
Siku hii pamoja na mambo mengine huwa ni utangulizi wa ya mahafali ya chuo hicho , kesho itakuwa ndio mahafali yenyewe . Hii itakuwa mahafali ya 15 tangu chuo hicho kutunukiwa ama kubadilishwa kuwa chuo kikuu kutoka iliyokuwa Taasisi ya mafunzo ya jamii Nyegezi (Nyegezi social training Institute NSTI) mwaka 1998.
Vituvo mbali mbali vimeshiriki shughuli hii ya leo vikiwemo Engineering, Mawasiliano ya Umma, Mahusiano ya Umma, Dini, Elimu, Sayansi ya jamii na Philosohpia.
Mgeni rasmi katika shughuli hii ya leo amekuwa na Askofu Ndimbo, Mwenyekiti wa Bodi ya chuo (SAUT), pamoja nae katika meza kuu alikuwepo Makamu mkuu wa chuo hicho Dkt Pius Mgeni, Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Dkt Thadeus Mukamwa na Dkt Helen , ambae ni mkuu wa masomo ya shahada za juu.
Hivihapa baadhi ya picha za tukio zima siku ya leo..

Naibu makamu mkuu wa chuo taaluma Dkt Mukamwa

Wataalamu wa picha mnato wakiwa kazini

Dkt Pius Mgeni

Sr Helen
 WATAALAMU WA MAJENGO NA UMEME


 BURUDANI KATIKA MASHAIRI NA UTUNZI TUNDUIZI...picha ya chini wataalamu hawa waliamua kucheza wimbo wa MAJANGA wa Snura

 WATAALAMU WA REDIO

 Chini: Bi Martha na Bwana Innocent wakiwa tayari kuelekeza uhariri wa picha za video

 KUKABIDHI SHAIRI KWA MGENI RASMI

Bi Ester Lymo, hapa akishughulika na kamera 
 Maelekezo kabla ya kuingia banda la PCCB na AISEC


 WATAALAMU WA SHERIA

 WATAALAMU WA USHAURI NASAHA KUTOKA HOSPITALI YA BUGANDO
 WATAALAMU WA UTETEZI WA UHAI - PRO LIFE

 WATAALAUMU WA MAZINGIRA
 WATAALAMU WA MAWASILIANO YA UMMA UPANDE WA REDIO
Bwana Haji Yona (mwenye sahati la draft) akitoa ufafanuzi juu ya utangazaji

Fr Mwanga Tiago, Joseph Kigingi (wa kwanza na wa pili kulia) wakitoa ufafanuzi juu ya uhariri wa vipindi vya redio


Mtaalamu kutoka kitengo cha mainjinia wa umeme akifafanua jambo

Bwana |Elia Migongo akimfafanulia mgeni rasmi juu ya urushaji wa matangazo katika redio

Bwana Said Lufune (aliyevaa Headphone) akitoa ufafanuzi juu ya uchanganyaji  wa picha katika luninga

Bwana Godfriend Mbuya(aliyekaa) hapa akimuelekeza mgeni rasmi na jopo lake juu ya usomaji wa habari wa luninga

No comments: