Thursday, August 29, 2013

TAARIFA KUBWA KWA JUMUIYA YA KIKRISTO LEO NI HII YA KIFO CHA ASKOFU MKUU WA KANISA LA EAGT Dkt MOSES KULOLA KUFARIKI DUNIA


Taarifa za hivi punde zinasema kuwa Askofu Mkuu wa Evangelistic Assemblies God Tanzania, Moses Kulola amefariki dunia takriban dakika 25 zilizopita. 
Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika kutoka kwa watu wa ndani wa familia hiyo, zinaeleza kuwa Askofu Kulola amefariki katika hospitali ya AMI (African Medical Investments) iliyopo Slipway jijini Dar es Salaam. 
Askofu Kulola, ambaye amezaliwa mwaka 1928, amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu na hata kufikia hatua ya kupelekwa nchini India kwa matibabu. 
Katika uhai wake, amepata watoto wengi wa kiroho ikiwemo Dr Daniel Kulola, Mchungaji Florian Katunzi, Zakaria Kakobe, Mzee wa Upako, Maboya, Mwasota na wengineo wengi. 
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina la BWANA lihimidiwe.

No comments: