Thursday, August 29, 2013

STORY KUBWA KUTOKA BUNGENI DODOMA HIZI HAPA

Story za Danson Kaijage, Dodoma
SAME MASHARIKI
MBUNGE wa Same Mashariki, Anne Kilango Mallecela (CCM)ameitaka serikali kubadilisha sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1995 ili kuwabana baadhi ya viongozi wanaotumia majukwaa kwa ajili ya kuleta uchochezi nchini.
Kilango alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kuihoji serikali kama hainoni kuwa kuna kila sababu ya kubadilisha sheria hiyo kwani ilikuwa ikiendana na siasa za mwaka huo lakini kwa sasa siasa zimebadilika sana je serikali haini umuhimu wa kubadilisha sheria hiyo ili kuwachukulia hatua baadhi yaw na siasa wakiwemo wabunge ambao wanatumia majukwaa ya siasa kusababisha uvunjifu wa amani.
ENDELEA KUZISOMA HAPA CHINI BOFYA "SOMA ZAIDI"
Kwa upande wage wa Mbunge wa Iramba magharibi Mwinguru Mchemba (CCM) alitaka serikali ieleze ni kwanini serikali kwa kutumia ushahidi uliopo wa baadhi ya wanasiasa kusababisha vifo vya watu mbalimbali katika mikoa mbalimbali wasichukuliwe hatua ikiwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe pamoja na katibu wake Dk.Willibroad Slaa ambao kwa sasa walikuwa wamewekwa jera kwa siku nyingi.
“Kwa kuwa majibu ya serikali yanasema kuwa ikithibitika kuwa wapo wanasiasa ambao wamesababisha machafuko watachukuliwa hatua na kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita wapo wana siasa waliosababisha vifa vya watu huko Arusha,Morogoro pamoja na mikoa nimgine na wapo watu wawaliosababisha kama serikali ingekuwa makini watu kama Mbowe na Silaa wamengekuwa Jera siku nyingi kabisa kabisa” alisema Mwigulu.
Awali katika swali la msingi la Mbunge wa Same Mashariki alitaka kujua kama serikali haioni kwamba sasa ni muhimu kuwanyang’anya viongozi wa siasa na wana siasa nafasi ya kazi ya siasa wale wanaokiuka maadili ya kazi ya siasa kama wale wanaoleta uchochezi unaosababisha kumwaga damu ya watanzania na kufanya vitendo vyote vinavyotishia amani ya watanzania.
Akijibu maswali hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais(Utawara Bora)George Mkuchika alisema kuwa Wizara imefanya mapendekezo ya sheria ya siasa ambayo itawasilishwa katika bungela Novemba mwaka huu.
Alisema sheria hiyo lengo lake kubwa ni kuipa meno ili kuwashughulikia wanasiasa ambao wanasababisha umwagaji wa damu pamoja na kusababisha vitendo vya uchochezi.
Hata hivyo alisema kuwa kwa sasa kiongozi wa kisiasa hachukuliwi hatua kunyang’anywa nafasi yake isipokuwa hatua au adhabu sitahiki zitachukuliwa dhidi ya kiongozi huyo pale tu chombo ama taasisis yenye mamlaka ya kutoa haki itapothibitishwa kuwa kiongozi huyo ni mkosaji wa kosa alilokuwa akituhumiwa kulitenda kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mkuchika alisema kuwa katika misingi ya Utawara bora na Utawala wa Sheria inataka kabla ya kumnyang’anya kiongozi nayetuhumiwa nafsi ya uongozi kuhakikisha kwamba upo ushahidi unaothibitisha makosa makubwa ya kukiuka maadili.
Mwisho. 
VITI MAALUM
MBUNGE wa Viti Maalum, Mariam Msabaha (Chadema) ameibana serikali ieleze ni mikakati gani wanaiweka kwa ajili ya kupambana na wafanya biashara ambao siyo waaminifu ambao wanatumia vipimo vya lumbesa kwa ajili ya kununua mazao ya wakulima.
Alitoa hoja hiyo jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kuelezwa ni hatua gani ambazo serikali inawachukulia baadhi ya wafanya biashara ambao wananunua mazao ya wakulima kwa kutumia vipimo ambavyo siyo sahihi.
 “Wapo wafanya biashara ambao wanawafuata wakulima mashambani mwao na kununua mazao kwa kujaza lumbesa wao wanaenda kuuza kwa faida kubwa ni hatua gani za serikali zinachukuliwa kwa watu hao ambao wamekuwa wakiwahujumu wakulima hao kwa kuwanyonya wakati wakulima wanatumia nguvu nyingi lakini hawapati faida” alihoji Msabaha.
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Tunduru Kusini Mtutula Mtutula (CCM)alitaka kujua kama serikali inatoa msisitizo wa kutumia mizani ya digitali kupimia zao la korosho kama ilivyo fanya kwa mazao mengine.
“Tatizo la wanunuzi wa mazao ya kilimo kuwapunja wakulima kupitia mizani ni kubwa si kwa wakulima wa pamba tu bali kwa wakulima wa korosho na mazao mengine je serikali haitoi msisitizo wa kutumia mizani ya digital kupimia zao la korosho kama ilivyo kwa mazao mengine” alihoji Mtutula
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Gregory Teu,alisema  ni kweli lipo tatizo kubwa la wanunuzi wa mazao ya kilimo kuendelea kupunjwa wakulima kupitia mizani zisizokidhi viwango.
Alisema uwa tatizo hilo si kwa wakulima wa pamba tu bali hata kwa wakulima wa korosho na mazao mengine.
Teu alisema kutokana na hali hiyo ni kosa kubwa kwa wanunuzi wa mazao kununua mazao kwa kutumia mizani ambayo haikubaliki ikiwa ni pamoja na kujaza lumbesa na badala yake wafanya biashara wa mazao wa nunue mazao hayo kwa vipimo ambavyo vinatakiwa.
Mwisho.
JIMBO LA TANDAHIMBA
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Samweli Sitta,amesema kuwa hadi sasa Kiswahili hakijatajwa katika mkataba kuwa lugha rasmi ya kutumika katika shughuli za Jumuiya.
Alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Tandahimba Juma Njwayo (CCM) aliyetaka kujua ni kwanini lugha ya Kiswahili inatumika katika Bunge la Afrika lakini haitumiki kwenye bunge la Afrika Mashariki (EALA).
Hata hivyo, Waziri huyo alisema kuwa hakuna sheria rasmi inayohalalisha lugha ya Kiswahili kutumia katika Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki na badala yake sheria inaitambua lugha ya Kiingereza.
Waziri Sitta alisema kuwa hadi sasa Kiswahili hakijatajwa katika mkataba kuwa ni lugha rasmi ya kutumika katika shughuli za Jumuiya hiyo.
“Kwa upande wa Umoja wa Afrika, Sheia iliyoundwa na umoja huo inaainisha katika Ibara ya 25 kuwa lugha zitakazotumika katika shughuli za Umoja huo ni lugha za nchi wanachama ambazo kwa sasa ni Kifaransa, Kireno, Kiingereza, Kiswahili na Kiarabu,” alisema Sitta.
Alisema kuwa Umoja wa Afrika unajumuisha lugha nyingi zaidi kuliko ilivyo kwa jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo inaainisha kuwa shughuli zake zote zinafanyika kwa lugha ya kiingereza.
  Wazori alisema hali hiyo ni ya mpito kutokana na baadhi ya nchi wanachama kutokuwa na uelewa wa kutosha wa lugha ya Kiswahili na kuepuka gharama za ziada za uendeshaji.
Kuhusu Burundi na Ruanda alisema nchi hizo zinatumia lugha ya Kifaransa tofauti na Tanzania na Kenya ambazo zinaendelea kusisitiza lugha ya Kiswahili.
VITI MAALUM
MBUNGE wa Viti Maalum Pauline Gekul (Chadema) ameihiji serikali kama hiko tayari kuwarudishia akina mama wajawazito ambao wananunua vifaa kwa ajili ya kujifungua kutokana na hospitali nyingi kutokuwa na vifaa hivyo.
Alitoa kauli hiyo jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza alipotaka kujua kana akina mama wajawazito ambao ulazimika kutoa fedha kwa ajili ya kununulia vifaa vya kujifungulia kutokana na kukosekana katika hospitali nyingi.
“Serikali mnachukua hatua gani kwa kuwarudishia fedha zao akina mama wajawazito ambao ulazimika kutoa fedha zao kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kujifungulia kutokana na kuwa akina mama wanatakiwa kujifungua bila kutoa gharama yoyote” alihoji Gekuli
Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali inawaadaa wananchi kwa kutoa majibu ya kuwa akina mama wajawazito wanatakiwa kupata huduma bure lakini Hazina imekuwa haipeleki fedha katika hospitali za Wilaya kwa ajili ya kunua madawa na vifaa tiba.
“Serikali imekuwa ikitoa kauli bungeni kuwa kima mama wajawazito kisera hawagharamii matibabu yao ya gharama za kujifungua,lakini kiuhalisia kina mama hao hulipia ghalama hizo..
“Je ni kwanini serikali inawahadaa wananchi kwa majibu hayo wakati wenyewe (Hazina) ndiyo chanzo cha tatizo kwa kutopeleka fedha hizo katika hospitali za Wilaya na nyinginezo” alihoji Gekuli.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dk.Seif Selemani Rashidi,alisema kuwa kwa mujibu wa sera ya afya ya mwaka 2007, serikali imeweka utaratibu wa kutoa huduma ya matibabu bila malipo kwa mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. 
JIMBO LA TARIME
 KATIKA kipindi cha awamu ya kwanza ya Miradi ya Millenium Co-Operation Challenge (MCC), ilitumia kiasi cha Sh 1,119,741,000,000 ambazo ni sawa na dola za Marekani 698,136,000 bungeni lilielezwa jana.
Naibu Waziri wa fedha Janeth Mbene alisema kuwa kati ya fedha hizo, kiasi cha Sh 1,010,208,000,000 zimetumika kuwalipa wazabuni mbalimbali ambapo makampuni ya wazawa yamelipwa kiasi cha Sh 24,678,000,000 na  kampuni za nje zimelipwa Sh 985,530,000,000.
Alikuwa akijibu swali la Nyambari Nyangwine (Tarime-CCM) ambaye litaka kujua ni utaratibu gani ambao unatumika kuwapa wazabuni wa tenda katika miradi ya MCC na ni kampuni zipi za Kitanzania na zipi za kigeni zilishinda zabuni hiyo.
Kingine alihoji pesa za miradi ya MCC zote zilikuwa kiasi gani na katika fedha hizo wazawa walipata kiasi gani na kama Serikali itakuwa na mkakati gani wa kuhakikisha fedha zote za misaada inayotolewa zinabaki nchini kwa wazawa.
Naibu Waziri alisema kuwa utaratibu unaotumika kuwapata wazabuni wa tenda katika miradi ya MCC nchini unafuata mwongozo wa manunuzi wa program za MCC, 2006-2009.
Alisema kuwa utaratibu huo hautoi upendeleo wa makampuni ya nchi iliyotoa fedha au nchi inayopokea.
Kuhusu idadi ya makampuni aliyataja kuwa katika kipindi hicho makampuni ya wazawa 203 yalishinda zabuni ya miradi ya MCC katika maeneo ya huduma za ushauri na vifaa ambapo makampuni 97 ya kigeni yalishinda zabuni kubwa katika maeneo ya wakandarasi na wahandisi washauri.
JIMBO LA CHONGA
WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Hawa Ghasia amesema zaidi Sh. Bilioni 3.3 zimekusanywa kama kodi ya maegesho ya magari Jijini Dar es Salaam katika kipindi cha Julai 2008 hadi Julai 2013.
Alitoa maelezo hayo jana bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Chonga, Haroub Mohamed Shamis (CUF).
Mbunge huyo katika swali lake Shamis alitaka kujua kiasi ambacho Serikali imekusanya katika Jiji la Dar es Salaam katika kipindi hicho.
Ghasia alisema kulingana na maegesho yaliyopo sasa na mkataba wa ukusanyaji mapato kiasi hicho cha Sh. Bilioni 3.33 ndicho kilichokusanywa.
Alisema katik kipindi cha mwaka 2008/2009 hadi 2011/12 jumla ya Sh. Milioni 606 zilikuwa zikikusanywa kila mwaka sawa na Sh. 50,500,000 kwa mwezi.
Alisema katika kipindi cha mwaka 2012/13 mapato ya amaegesho yaliyokusanywa yalikuwa  Sh. Milioni 910.02.
“Mwaka 2012/13 mapato yaliongezeka kutokana na mwekezaji kuongezewa kiasi cha fedha ambazo anatakiwa kukusanya kutoka Sh. Milioni 50.5 hadi Sh, milioni 75.83  kwa mwezi,” alisema Ghasia.
Alisema mapato yote hayo hugawanywa kwenye halmashauri zote za Jiji la Dar es Salaam.
JIMBO LA MBEYA MJINI (Michezo )
MBUNGE wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu ameibana serikali ieleze ni kwanini mpaka sasa stika za TRA hazitumiki katika kazi za wasanii.
Aidha alisema kuwa serikali haina dhamira ya kweli ya kuwasaidia wasanii nchini na ndiyo maana wanaibiwa kila kukicha kwani hata kampuni za simu haziwalipi wasanii kutokana na milio wanaoitumia katika simu hizo.
Mbilinyi alitoa kauli iyo jana bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kuitaka serikali ieleze ni hatua gani zinachululiwa kwa makampuni ya simu kuhusu wizi wanaowafanyia wasanii wengi nchini kwa kutumia nyimbo zao katika milio ya simu lakini hawalipwi.
Mbali na hilo aliitaka serikali hiunde timu huru ya kuchunguza na kujiridhisha ni kiasi gani cha wizi ambao unafanywa na makampuni hayo badala ya kuwataka wasanii wenyewe wafuatilie ili kujua ni jinsi gani wanavyoibiwa kazi zao na makampuni hayo.
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Kigoma Kaskazini,Zitto Kabwe (Chadema) alitaka kujua kiasi ambacho kampuni za simu kiliingiaza kama pato ghafi kutokana na kuuza kazi za wasanii kupitia miito ya simu katika mwaka ulioishia Desemba 2012 na asilimia ngapi ilibaki kwa msanii na asilimia iliyobaki kwa kampuni husika.
Mbunge huo pia alitaka kujua lini Serikali itatunga kanuni za kuweka wazi mapato ya kazi za sanaa kwa kampuni za simu na kiwango cha chini cha mtanzania kulipwa kutokana na pato ghafi.
Akijibu swali hilo Naaibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknologia,January Makamba alisema  hakuna taarifa mahsusi za pato ghafi lililotokana na kuuza milio ya simu kwa kuwa mauzo ya makampuni ya simu hutokana na huduma za bidhaa mbalimbali.
Alisema katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika usambaji kazi za wasanii kupitia simu za mkononi, wizara iliitisha kikao cha wadau na kuunda kamati iliyoshirikiwa wadau mbalimbali.
“Pamoja na mambo mengine kamati hiyo imeazimia kuweka utaratibu wa kuifanyia marekebisho Sheria za COSOTA na kwamba COSOTA izichukulie hatua za kisheria kampuni zinazowalipa wasanii chini ya kiwango kilichowekwa kisheria,” alisema.
 Wakati huo huo mbunge wa Ilala, Mussa Zungu Azzan (CCM) ametaka Serikali kuchukua hatua za haraka kukomesha tabia ya makampuni ya simu ya kuwaibia wateja wake.
Akiuliza swali la nyongeza bungeni jana, Zungu alisema wizi huo unatokana na kampuni hizi kuwaunganisha wateja wa simu huduma ambazo wanatakiwa kuzilipia bila ridhaa yao.
Alisema tabia hiyo ni wizi na kwamba makampuni hayo yanapata fedha nyingi kupitia huduma hizo za lazima.
“Lini Serikali itakomesha tabia hii ya wizi unaofanywa na kampuni za simu za kuwalazimisha wateja kutumia huduma bila ridhaa yao?” alihoji Zungu.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba alisema Serikali kuptia Mamlaka ya Mawasiliano itakaa na kuandika kanuni mpya ambazo zitadhibiti mapungufu hayo.
Alisema pia Serikali itaifanyia marekebisho  Sheria ya Mawasiliano (EPOCA) ili kuyabana makampuni yaweze kutoa huduma bora na kutowaibia wateja.

JIMBO LA KONDE

NAIBU Waziri wa Nishati na Madini Stephene Masele,amesema kuwa vituo 78 vya mafuta pamoja na magari 4 ya kubeba mafuta yalikamatwa kati ya mwaka 2010 na 2012 yakishusha mafuta nchini yaliyopaswa kwenda kuuzwa nchi za nje.
Kauli hiyo aliitoa jana bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Konde Khamisi Said Haji (CUF).
Mbunge huyo alitaka kujua serikali imefanikiwa kiasi gani kudhibiti mianya kudhibiti ya upotevu wa mapato hususani kwa bidhaa za mafuta.
Aidha alitaka kuelewa ni makampuni mangapi yamekamatwa mwaka 2010 -2012 yakihusisha mafuta ya transifoma hapa nchini na hatua gani zimechiyo mafuta

No comments: