Thursday, August 29, 2013

PICHA KUMI ZA AJALI YA BASI JIRANI NA MTWARA GIRLS LEO HII ASUBUHI 28 WAJERUHIWA

 KUTOKAHOSPITALI YA MKOA, LIGULA, Majeruhi 28 wamepokelewa hospitalini hapo na kutibiwa. Dr Gwao, ameiambia blog hii kuwa jumla ya majeruhi 21 wametibiwa na kuruhusiwa, kwa mujibu wa Dr Gwao, hakuna madhara makubwa , mtu mmoja mwenye umri wa miaka 65 ndiye alieumia zaidi ambapo amevunjika mkono na juhudi za kumsafirisha kumpeleka Dar es salaam kwa aajili ya upasuaji tayari zinafanyika, mgonjwa mdogo kuliko wote anaumri wa miaka 8 na ni wa kiume. 
Basi hilo lilikuwa linatokea Newala kwenda mkoani Mtwara, linafahamika kwa jina la IBRA EXPRESS T 950 BMY.
KUTOKA KWA MASHUHUDA, Basi hilo lilipofika eneo la tukio, gari jingine ambalo lilikuwa limebeba mchanga lilijitokeza na kulivuka basi la abiria (over take), na ghafla likasimama mbele hali iliyopelekea dereva wa basi kuanza kufanya juhudi za kunusuri ajali hiyo lakini bahati mbaya haikufanikiwa.

MAHOJIANO, Mwandishi wa habari wa kujitegemea Bw Majani , akizungumza na Idrisa Bandali..
SIKILIZA MAHOJIANO HAPA

No comments: