Saturday, August 10, 2013

STORY YA MUJINI KUHUSU EID

WAISLAMU WOTE DUNIANI JANA WANAADHIMISHA SIKUKUU YA EID EL FITRI AMBAPO WAISLAMU WOTE WILAYANI KAHAMA WANAUNGANA NA WAISLAMU WENZAO DUNIANI KOTE KUSHEREHEKEA SIKUKUUU HIYO.
SALA YA EID IMEFANYIKA ASUBUHI HII KATIKA VIWANJA VYA SHULE YA KAHAMA MUSLIM IKIONGOZWA NA SHEKH WA WILAYA YA KAHAMA, SHEKH OMARY DAMKA, AMBAYE AMEWATAKA WAISLAM KUSHEREHEKEA KWA AMANI NA KUACHANA NA MATENDO YASIYOMPENDEZA MUNGU.
SHEKH DAMKA AMESEMA SIKU YA EID NI SIKU YA WAISLAMU KUSAIDIANA NA AMEWATAKA WAISLAMU KUENDELEZA IBADA HATA BAADA YA KUKAMILIKA KWA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHAN, NA KWAMBA SALA HIYO ITAFUATIWA NA BARAZA LA EID KATIKA VIWANJA HIVYO.
KITAIFA SALA YA EID IMESALIWA KATIKA UWANJA WA ALI HASSAN MWINYI MKOANI TABORA IKIONGOZWA NA MAKAMU WA RAIS, DK GHARIB BILAL, AMBAPO BAADAE ITAFUATIWA NA BARAZA LA EID LITAKALOSHIRIKISHA VIONGOZI MBALIMBALI.
MKUU WA MKOA WA TABORA, FATMA MWASSA AMELISHUKURU BARAZA KUU LA WAISLAMU TANZANIA, BAKWATA KWA KUIFANYA SIKUKUU YA EID EL FITR KITAIFA MKOANI TABORA.
PICHA KUTOKA MICHUZI BLOG

No comments: