Saturday, August 10, 2013

KUTOKA MUSOMA... HIZI NDO HABARI

MUSOMA. WAKATI SERIKALI IKISISITIZA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO KUTOTOZWA FEDHA KATIKA VITUO NA HOSPITALI ZOTE ZA SERIKALI,IMEBAINIKA KUWA BADO BAADHI YA VITUO VYA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA MKOANI MARA VIMEZIDI KUKAIDI AGIZO HILO.
WAKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI BAADHI YA WANAWAKE WAJAWAZITO NA WAZAZI WANAGUZA WATOTO KATIKA HOSPITALI YA MKOA WA MARA,WAMESEMA LICHA YA SERIKALI KUTOA TAMKO LA MATIBABU KWA MAKUNDI HAYO KUTOLEWA BURE LAKINI BADO WAMEENDELEA KUTOZWA FEDHA.
WAMESEMA WANAWAKE HAO WAJAWAZITO WAMEKUWA WAKITOZWA SHILINGI ELFU TANO KWAAJILI YA KUNUNULIA VIFAA NA SHILINGI ELFU MBILI KWAAJILI YA KULIPIA FAILI HUKU WATOTO WADOGO WAKITOA SHILINGI ELFU MBILI KWAAJILI YA FAILI PAMOJA NA KUTAKIWA KUTOA FEDHA ZA KUNUNULIA DAWA.
MWENYEKITI WA BODI YA HOSPITALI HIYO YA SERIKALI MKOANI MARA ASKOFU AMOS MUHAGACHI,AKIZUNGUMZA NA RADIO ONE STEREO,AMESHANGAZWA NA WAAUGUZI HAO KUWATOZA FEDHA WAJAWAZITO NA WATOTO WADOGO IKIWA NI KINYUME NA MAELEKEZO YA SERIKALI.
HATA HIVYO AMESEMA KAMWE BODI YAKE HAITAWAVUMILIA UKIUKWAJI NA KUPUUZA WA MAELEKEZO YA SERIKALI NA KUAHIDI KUCHUKUA HATUA KALI KWA WOTE WATAKABAINIKA KUFANYA VITENDO HIVYO.
BUTIAMA SERIKALI WILAYANI BUTIAMA MKOANI MARA IMETANGAZA KUFUNGWA KWA MASOKO NA MINADA YOTE NDANI YA WILAYA HIYO PAMOJA NA KUZUIA UKUSANYAJI WA USHURU HADI ITAKAPO JIRIDHISHA MAENEO HAYO YAMEFANYIWA USAFI WA KUTOSHA. HATA HIVYO UONGOZI HUO WA SERIKALI YA BUTIAMA,UMESEMA ITARUHUSU MASOKO NA MINADA HIYO KUENDELEA NA SHUGHULI ZAKE BAADA WAHUSIKA KUFANYA USAFI HUO NA KWAMBA KATIKA KIPINDI CHA WIKI MBILI LAZIMA MAENEO HAYO YOTE YAWE YAMETEKELEZA AGIZO. MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA BI ANGELINA MABULLA,AMETANGAZA UAMUZI HUO KATIKA SOKO LA BUTIAMA,AMBAPO AMEWATAKA VIONGOZI WA SERIKALI ZA VIJIJI HUSIKA KUSIMAMIA ZOEZI HILO LA USAFI HUKU AKIZUIA WAFANYABIASHARA KUACHA KUTOA USHURU HADI USAFI HUO UWE UMEFANYIKA. NAO BAADHI YA WAFANYABIASHARA WA SOKO HILO LA BUTIAMA WAMEUNGA MKONO AGIZO LA MKUU WA WILAYA YA BUTIAMA HUKU WAKISEMA HALMASHAURI IMEKUWA IKIKUSANYA USHURU LAKINI BILA KUSAFISHA MAZINGIRA YA SOKO HILO PAMOJA NA KUTOKUWEPO KWA CHOO KATIKA ENEO HILO. HATA HIVYO BAADA YA AGIZO HILO LA MKUU WA WILAYA AMBALO AMETOA CHINI YA ULINZI MKALI WA POLISI,VIONGOZI WA SOKO HILO WAMELAZIMIKA KUSIMAMISHA KWA MUDA BIASHARA KATIKA SOKO HILO NA KUANZA KUFANYA USAFI MARA MOJA.

STORY ZOTE NA AHMAD NANDONDE

No comments: