Tuesday, August 6, 2013

TAKWIMU MPYA ZA UKIMWI, MKOA MPYA WA NJOMBE UNAONGOZA, IRINGA YA PILI

TUME ya Kudhibiti UKIMWI nchini (TACAIDS)imesema mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na maambukizi makubwa ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimia 14.8 ikifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1.
Mkoa wa Mbeya unashika nafasi ya nne (9) Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dares Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera(4.0)na Geita (4.7). Mara (4.5), Mwanza (4.2),Mtwara (4.10), Kilimanjaro (3) Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3., Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya UKIMWI yamepungua kwa kasi ndogo.

No comments: