Friday, August 16, 2013

WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA SUALA LA ULINZI

Story Ahmad Nandonde MUSOMA.
KUFUATIA KUWEPO KWA MATUKIO MBALI MBALI YA UHALIFU MKOANI MARA WANANCHI WILAYANI BUTIAMA WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWA HALI NA MALI KATIKA SUALA ZIMA LA ULINZI NA USALAMA.
HAYO YAMESEMWA NA MKUU WA WILYA YA BUTIAMA BI. ANGELINA MABULA KATIKA HOTUBA YAKE ALIYOITOA KATIKA KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI YA HALMASHAURI YA WILAYA DCC KILICHOFANYIKA LEO KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUTIAMA.
AMESEMA KUMEKUWA NA MATUKIO MENGI YA UHALIFU AMBAYO YAMEKUA YAKITIA AIBU HIVYO KUWATAKA WAJUMBE KUWAHAMASISHA WANANCHI JUU YA USHIRIKI WAO KIKAMILIFU KATIKA SUALA LA ULINZI NA USALAMA IKIWA NI PAMOJA KUTAMBUANA NA HATA MGENI ANAPOINGIA NI VYEMA AKAHOJIWA ILI KAMA KUTAKUWA NA UHUSIANO WOWOTE NA MATUKIO YA UHALIFU BASI IWE RAHISI KUKAMATWA.
BI. MABULA AMEONGEZA KUWA ILI JAMII IWE KATIKA HALI YA USALAMA NI DHAHIRI KWAMBA KUNAHITAJIKA KUWEPO NA USHIRIKIANO NA USIRI KATIKA UTOAJI TAARIFA PAMOJA NA UTAYARI ILI KUHAKIKISHA MATENDO YA UHALIFU YANAKOMA IKIWA NI PAMOJA NA KUONDOKANA NA TABIA ZA WATU KUIJICHUKULIA SHERIA MIKONONI MWAO.
KWA UPANDE WAKE KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM WILAYANI BUTIAMA BI. MERCY MARAMBO AMESEMA KUTOKANA NA TABIA YA WATUHUMIWA KUACHILIWA HURU MUDA MFUPI KABLA YA SHERIA KUCHUKUA HATUA KWAKISINGIZIO CHA KUTOPATIKANA USHAHIDI WA KUTOSHA AMEMUOMBA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYOTE VINAVYOSIMAMIA MHIMILI WA SHERIA NCHINI, KUTAFUTA NJIA MBADALA ITAKAYOELEKEZA VYEMA ILI WALE WOTE WANAOFANYA HIVYO WAWEZE KUCHUKULIWA HATUA KALI.
NAYE MRAKIBU MWANDAMIZI WA JESHI LA POLISI WILAYANI HUMO SSP. AUDAX MAJALIWA AMEWATAKA WATENDAJI WA KATA, TARAFA, NA VIJIJI KUHAKIKISHA WANAWASHUGHULIKIA IPASAVYO WALE WOTE WATAKAOKIUKA KUSHIRIKI KATIKA ULINZI SHIRIKISHI KWA KUWAFIKISHA KATIKA VYOMBO VINAVYOHUSIKA ILI SHERIA IWEZE KUCHUKUA MKONDO WAKE.

No comments: