Friday, May 10, 2013

BONANZA LA KUMUAGA DKT KITIMA, KAMA HUKUHUDHURIA MECHI HIZI PICHA ZAKUFAA

HII LEO katika chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, SAUT , kumefanyika bonanza la aina yake kwaajili ya kumuaga aliyekuwa makamu wa chuo hicho kikuu na kikongwe hapa nchini , mkuu huyo anamaliza muda wake wa utumishi. Bonanza hilo pia lilikuwa maalumu kwaajili ya kumtambulisha makamu mkuu wa chuo mpya Padre Dkt. Mgeni
Wa Kwanza hapa kushoto ni Dkt Mgeni, huyu ndie mrithi wa Dkt Charles Kitima anaemaliza muda wake siku chache zijazo.

Kwenye mechi ya mpira wa Kikapu, kati ya Mapadre wa Jimbo na wale wa SAUT

 MGENI RASMI, Dkt Charles Kitima, wakati alipokuwa akiwasalimia wachezaji, kabla ya mchezo maalumu wa kumuaga kama makamu mkuu wa chuo kikuu SAUT, leo hii.
 Mara baada ya kuzindua mpambano huo hapa Dkt Kitima na meza kuu wakielekea kuchukua nafasi zao
 VYENGA KWA KWENDA MBELE, mchezaji wa mapadre wa SAUT (Mwenye jezi za blu bahari) akimtoka beki wa mapadre wa jimbo.
KUTESA KWA ZAMU

UMAHIRI, mshambuliaji wa mapadre wa Jimbo akiumiliki vyema mpira

BAADAE: Mechi hiyo ambayo ilichezwa kwa dakika 60, huku wahubiri hawa wote wakionekana kulijua vyema gozi lang'ombe, dakika zote za mchezo zilimalizika kwa sare tasa...KISHA mikwaju ya penalti ikawapa ushindi mapadre wa SAUT kwa penalti 6 kwa 5.

Mfungaji wa goli la ushindi akiwa amebebwa juu juu

HONGERA KWA UMAHIRI, Fr Maziku , akiwa nampongeza golikipa wa timu ya mapadre wa SAUT... mara baada ya kuonesha umahiri katika kuzicheza penalti tatu.

Mshereheshaji katika shughuli hii ya Leo alikuwa Chilwa Chiwiko.

No comments: