Tuesday, April 30, 2013

WANANCHI TOENI TAARIFA POLISI


Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA
JESHI LA POLISI MKONI MARA LIMEWATAKA WANANCHI KUTOJICHUKULIA SHERIA MKONONI NA WATOE TAARIFA ZA SIRI KWA JESHI HILO ILI KUWABAINI WOTE WANAOHUSIKA NA VITENDO VYA KIKATILI DHIDI YA BINADAMU.
HAYO YAMESEMWA NA KAMANDA WA JESHI LA POLISI ABSALOM MWAKYOMA WAKATI AKITOA TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKANA NA MAUAJI YALIYOFANYIKA ENEO LA BUHARE -MGARANJABO, MANISPAA YA MUSOMA AMBAPO MTU MMOJA AMBAE HAKUFAHAMIKA KWA JINA AMEUAWA NA WATU WASIOJULIKANA 
AMESEMA MWILI WA MAREHEMU HUYO AMBAYE NI MWANAMKE ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 20 NA 25 UMEKUTWA UKIWA UMETELEKEZWA KARIBU NA MFEREJI WA MAJI JIRANI NA ENEO LA KUCHIMBA MCHANGA UKIWA UMEACHWA UCHI NA WAUAJI HAO 
AMEONGEZA KUWA CHANZO CHA KIFO HICHO BADO KINACHUNGUZWA NA KUIAMURU SERIKALI YA KIJIJI CHA BUHARE KUIZIKA MAITI HIYO.
HATA HIVYO KAMANDA MWAKYOMA AMESEMA KUWA HAKUNA MTU ALIYEKAMATWA KUHUSIANA NA TUKIOA HILO NA KUWAOMBA WANANCHI KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ILI KUWABAINI WOTE WANAOHUSIKA NA UHALIFU ILI WAWEZE KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA

No comments: