Friday, March 22, 2013

HOTUBA YA RAIS WA WANAFUNZI SAUT MWANZA, WAKATI ALIPOVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI NA BUNGE

Kwanza kabisa natoa shukrani za dhati kwa wanafunzi na wafanyakazi wa Chuo hiki kwa ushirikiano mkubwa mlionipatia kwa kipindi changu cha mwaka mmoja wa uongozi. Nimejifunza mengi ndani na nje ya nchi. Hakuna uongozi usio na changamoto lakini ukimtumainia Mungu atakushindia yote.
Nafurahi kuwa naondoka kwny uongozi nikiwa nimetekeleza ilani yng ya uchaguzi almost 90% yaniliyoahidi. hiyo ni level ya juu sana ktk political archievement.
Baadhi ya niliyoahidi ni kama ifuatavyo.
1.Tumefanikiwa kurekebisha sound system za madarasani na projectors. naamini mmejionea wenyewe kazi iliyofanyika na hakuna darasa linasumbua.
2.Tuliahidi umeme wa uhakika Library, na nimepambana sana kwny vikao vya maamuzi ndani ya chuo ikiwemo,
-University senate
-managament Board,
-university council kupeleka hoja ya kuhakikisha inatengwa bajeti ya kutekeleza hilo.
Jitihada hizo zikazaa matunda na tayari zimenunuliwa solar panels zaidi ya 70 na zimeanza kufungwa ili library iwe na reliable source of energy. Nafarijika kwamba sasa wanafunzi wakiwa Library umeme ukakatika hawatafukuzwa tena kama ilivyokuwa awali.
3.Tulipinga Serikali ya wanafunzi (sautso) kuwa na vyumba vitatu vya ofisi na nikaahidi kupigania ofisi mpya. Na tumepata ofisi mpya near Mwanjonde Building.


Tayari tumeikarabati kwa kuboresha system ya choo, kuweka milango, na kuvunja baadhi ya kuta ili ionekane ofisi badala ya nyumba ya kuishi. Tumeweka mashelf. Kwa kifupi ukarabati ndani umemalizika hadi rangi, bado nje.

Japokuwa ofisi imeshindwa kukamilika kwny uongozi wetu lakini nafarijika kuwa serikali ijayo itakuwa na ofisi mpya ambayo ni matunda ya juhudi zetu. Ofisi hii ina vyumba 6 na ile ya zamani ina vyumba 3, hvyo kwa ujumla SAUTSO itakuwa na vyumba 9 vya ofisi na kuwa Serikali pekee ya wanafunzi yenye ofisi nyingi zaidi Tanzania.

4.Tuliahidi kuboresha mazingira ya kusomea nje ya madarasa. Tulijitahidi kutafuta ufadhili ndani na nje ya chuo na hatimaye tukafanikiwa kukutana na shirika maendele la ujerumani ambao wameingia ubiya (patnership na TiGo) ktk kutusaidia.

As the result wamekubali kutujengea vimbweta vya kusomea vya kisasa na kuboresha vilivyopo, kuanzid eneo la ATM hadi near madarasa ya M10 na M9.

Huu ni ufadhili mkubwa maana mradi huu utagharimu jumla ya sh. Mil.79. Tayari mradi umepata baraka za Vice Chancelor na tumeshasign mkataba wa kuwaruhusu kuanza kazi.

Pamojaa na pongezi kubwa tulizozipata kwa Vice Chancelor kutokana na jitihada zetu, tunaiasa serikali ijayo itoe ushirikiano wa kutosha kuhakikisha mradi huu unaanza kutekelezwa. kumbukeni mkilalala wanaweza kuona hamna nia hivyo hivyo wakakata tamaa.

6.Tumepigania wanafunzi 16 waliofukuzwa chuo kurudishwa masomoni baada ya kutetea rufaa zao kwenye Board of Appeal. Mmojawapo ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha wanafunzi wanaosoma Kiswahili (CHAWAKAMA). Pia tulijitahidi kuwaombea msamaha wanafunzi zaidi ya 260 wa Public Relations ambao management ilishauri wafukuzwe kutokana na kufanya fujo kwny chumba cha mtihani. We pled for clemency na wote wakasamehewa.

7.Tumepunguza matumizi ya SAUTSO na kureduce budget kutoka mil.240 za serikali iliyopita kufikia mil.136 kwa serikali yng.

8.Tumeratibu kwa ufanisi safari ya Rwanda kwa washindi wa Fawasco mwaka jana. Pia tulifanikiwa kupeleka timu 4 kwny SUSAUT Gathering ya Morogoro (awali zilikuwa zikienda timu 2 tu, yaani football na netball. Lakini chini ya uongozi wetu tumefanikiwa kuongeza timu ya Basket ambayo ilichukua ubingwa kwa kuvifunga vyuo vingine zaidi ya 10 vilivyoshiriki. Timu yetu ya Basket ndio timu pekee ambayo haikuwahi kupoteza mchezo wowote tangu mwanzo hadi mwisho.
Laiti tusingeipeleka ushindi huo tusingeupata.

Pia timu ya Voleyball ambao nao tuliwapeleka wakashiriki kwa mara ya kwanza, waliingia fainali na kuibuka washindi wa pili.

9.Tumeandaa makongamano na forums mbalimbali zenye manufaa kwa wanachuo kama:
-Forum ya katiba ambapo tulikuwa na Deus Kibamba (m/kiti Jukwaa la Katiba)

-Forum ya maadili ya waalim ambapo tulikuwa na Rais wa chama cha waalimu Adrian Mkoba,

-forum ya siku ya siku ya wanawake duniani ambapo tulimwalika Prof.Anne Tibaijuka lakini unfortunately akashindwa kufika,

-Na wakati wa kuvunja serikali last saturday tulihitimisha na forum ya uchumi ambapo tulikuwa na Mh.Tundu Lissu na mkurugenzi wa TPDC.

Forum zote hizi zimesaidia sana kuongeza upeo wa wanafunzi wetu ktk mambo mbalimbali na kupata fursa ya kuuliza yale yaliyokuwa yakiwatatiza.

10.Tumeboresha mashindano ya fawasco kwa kutafuta udhamini NMB na TiGo.

NMB wametoa jezi, mipira, usafiri wa timu kwenda kambini. In advance pia watatoa flat screen mbili za inch 52 kwa SAUTSO ijayo. Tayari tumeshasign mkataba ndio maana uwanja wa Raila Odinga unashine kwa flies za NMB.

Hizo ni juhudi zetu kama Serikali yetu inayoondoka madarakani. Awali mimi na wizara yangu ya michezo tulikutana na Mkurugenz wa NMB Lake zone Mr.Straton Chilongola na baadae tukakutana na Mkurugenz wa Masoko NMB taifa Mr.Imani Kajula ktk kutekeleza azma hiyo.

In return NMB tumekubali wafungue ATM yao hapa chuoni ili kutengeneza two ways symnentrical function ktk CSR. Natumaini mmeiona ATM hiyo na kwa wateja wa NMB anzeni kuitumia kwa ari, nguvu na kasi zaidi.

Tunafarijika kuona ATM ya NMB iliyotokana na juhudi zetu, lakini tunafarijika zaidi kuona wachezaji wetu wakiwa wanapendeza kwny jezi za NMB.

TIgo wao watachangia Mil.6 kufanikisha Fawasco ya mwaka huu na tayari wamekabidhi kwa utawala (mbele ya DVCAF) vifaa vyenye thamani ya mil.3.5. Tigo pia watafanya tamasha kubwa siku ya fainali ambapo wamedai kumleta msanii wa kimataifa (watamtaja badae)

kwa ujumla ufadhili wa Tigo na NMB utakagharimu takribani mil.15. Haya ni mafanikio makubwa sana kwetu, kwa management na kwa wanafunzi wote kwa ujumla. Hakuna serikali iliyowahi kufanya hivi. Wakati wengine walikuwa wanaomba fedha management, sisi tumetafuta fedha kwa asasi za nje na kuzileta management. Hizi juhudi zinazopaswa kupongezwa na kila mpenda maendeleo.

11.Tumehakikisha fedha za meals & Acomodation zinafika kwa wakati, (unless kwa wale wachache waliokuwa na special case).
Pia hii ni serikali pekee ambayo imehakikisha fedha za Research zinafika kwa muda muafaka (kabla wanafunzi hawajafanya mitihani yao ya mwisho).

12.Tuliahidi bei ya chakula itabaki kuwa 1200 kwa 1500 na tumehakikisha hilo limetekelezwa. Kuna kipindi wazabuni walipandisha bei kinyemela kufikia sh.2000 kinyume na mikataba yao ya zabuni kwa kulalamikia cost of production. Lakini tuliunda kamati maalum iliyofanya uchunguzi wa kina juu ya madai hayo na kubaini kuwa madai hayo hayakuwa na ukweli wowote.
Hivyo tukalazimika kutoa notice ya saa 24 kwa wazabuni kurudisha bei ya kawaida .(1200 kwa 1500). Tunawashukuru kwa kutii agizo hilo na kurudisha bei ya kawaida kama ilivyoelekezwa ktk mikataba yao.

Yamkini tuliibua migogoro na baadhi ya wazabuni (hatuna budi kuomba radhi) lkn nia yetu ilikuwa kulinda haki za waliotuchagua.

Kwa kifupi tumefanya mengi, we cnt explain each &everything but tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kutimiza yale tuliyoahidi.

Kama kuna ambayo tumeacha tunaamini watakaokuja nao watafanya kwa nafasi yao.

Nitumie pia fursa hii kuipongeza Tume ya uchaguzi iliyoundwa jumamosi na kuapishwa juzi na mwanasheria mkuu wa chuo. Nimpongeze Mh.Lumuli Makala kwa kuchaguliwa M/kiti wa Tume. Naamini yeye na jahazi lake wataongoza tume ktk kufanya uchaguzi huru na haki na kumpata Rais ambaye ni chaguo la wana-SAUT.

Nitoe shukrani za pekee kwa baraza langu la mawaziri ambalo kila mmoja amepigana kiume kuhakikisha anawatumikia kwa ufanisi watu wa SAUT.

Nimshukuru Makamu wangu Consolatha Michael, Waziri Mkuu Baraka Mnkeni na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Nice Mberesero kwa kunishauri kwa busara ktk kipindi chote cha uongozi wangu.

Nimshukuru Spika wa Bunge la SAUTSO Mh.Lutehanga Eric kwa kuongoza bunge kwa hekima na kuhakikisha bunge linatimiza kazi yake ya kuisimamia serikali.

Zaidi ya yote nimshukuru Makamu Mkuu wa chuo Rev.Dr.Charles Kitima kwa ushirikiano mkubwa kwa SAUTSO. Kila ninapokuona naona matumaini. Nikushukuru pia kwa kutusaidia kufanikisha safari ya SAUTSO Zambia, Malawi Rwanda na kwingineko. Mungu akubariki sana. Hakika wewe ni mfano wa kuigwa.

Niushukuru uongozi wote wa chuo kwa ujumla wake, kwa kuanzia na DVCAA, DVCAF, Mwanasheria Mkuu wa Chuo na Dean of students kwa kutusaidia kila tulipokwama. Hawakuchoka tulipohitaji msaada wao.

kwa moyo wa dhati niwashukuru waalimu wangu walioniwezesha kufika hapa, na hata nilipokuwa kiongozi hawakuniacha bali walizidi kunishika mkono na kuniongoza pale nilipoteleza.

Angalau kwa kuwataja wachache japo waalimu wangu wote wamekuwa kiungo kikubwa kwangu kufika hapa nilipofika.
Madam Duwe, Mr.Alute, Mr.Mpagaze, Mr.Tibaijuka, Madam Sakina, Madam Joan, Madam Mpuya, Rev.Maziku, Rev.Wagana, madam Bhoke, Mr.Kopoka, Mr.Nkwabi, Mr.Shao na wengine. Im realy proud of you dear teachers, for your hardwork to shape my personality.

Siwezi kuwasahau waalimu wangu pia shule ya msingi na sekondari, hasa Mwal.Fitris Tarimo wa Majengo sekondari aliyeiona nyota ya uongozi ndani yng tangu mapema.

Nitakuwa mchoyo wa fadhila bila kuwashukuru wanadarasa wenzangu wa B.A in Mass communications kwa ushirikiano mkubwa walioonesha tangu wakati wa kampeni hadi sasa. Hawakuchoka kunishauri, kunionya nilipokosea, kunielekeza. Hata nilipozidiwa na majukumu na kushindwa kufika darasani bado walijitoa kunisaidia.

Bro.Msengezi, mbunge wangu Luther, pacha zangu Thom na Hans, mpiganaji wangu Mponjoli, Mandawa Kevy, Sylvester, Kalisa,Akida, Chilwa,
kaka zangu Mapuli, Maziku etc, dada zangu Gloriana, Nancy, Cathy, Sr.Lekule, Zulfa, Angel na wanadarasa wote kwa ujumla. I realy appreciate u guys.
Nice to tell u kuwa majukumu yamepungua, safari nazo ndo zinaishiaishia, sasa darasani kama kawaida, ktk kuboresha GPA.

Pia shukrani hizi ziwafikie wanafunzi wote wa SAUT.

Wa mwisho japo ni wa kwanza kwa umuhimu ni wazazi wangu Mr&Mrs Malisa Joseph Elisante.

Zaidi ya wote ni Mwenyezi Mungu wa mbinguni kuniumba na kuwa nami ktk kila hatua ya maisha yng,
leo nimekuwa Kiongozi wa SAUTSO, kiongozi wa shirikisho la vyuo vikuu vya SAUT na kiongozi wa shirikisho la wanafunzi vyuo vikuu Afrika Mashariki kwa uweza wako Mungu. Wewe ndiwe ujuaje nitokako na ninakoelekea, uniongoze kuzifikia ndoto zangu. Wewe husema iwe ikawa, sifa na utukufu vikurudie (Zaburi 8:1-8).

WITO KWA SERIKALI IJAYO.
Uongozi ni kujitoa sadaka, uongozi ni kujinyima, Uongozi wa kweli ni mzigo. Kuna wakati utalazimika kuacha jambo hata kama unalipenda kwa sababu wewe ni kiongozi, na kuna wakati utalazimika kufanya jambo hata kama hupendi ili kuwatumikia watu.

Ukiwa kiongozi utapoteza masomo, utakosa muda wa kufanya mambo yako binafsi, utakosa quiz, assignment kwa ajili ya kuwatumikia watu. GPA yako itatetereka kwa ajili ya utumishi uliotukuka. Kuna wakati utatumia hadi fedha zako binafsi ili mambo yasikwame, kuna wakati utakosa hata muda wa kula, muda wa kulala, pengine hata muda wa kujisomea lakini ni wachache sana watakaoappreciate juhudi zako.

Usife moyo, usikate tamaa, songa mbele ukimwomba Mungu. Wapo watakaokudisappoint kwa kukosa fursa may be ya uwaziri na kudiscredit kila unalofanya lakini usikate tamaa.

Unaweza kukosa muda wa kufanya jambo lolote binafsi. Muda wa kula, muda wa kuwajulia hali ndugu zako (wengine kwa kutokujua watasema unaringa baada ya kuwa kiongozi), unaweza kukosa hata muda wa kulala, lakini jitahidi usikose muda wa kufanya mambo mawili makubwa:
1.Muda wa kusali
2.Muda wa kufanya kilichokuleta chuoni (kusoma). Hata kama utapata muda kidogo, utumie vzr.

WANA SAUT,
NAWATAKIA UCHAGUZI HURU NA WA HAKI WENYE AMANI. MUNGU AWABARIKI WOTE.

No comments: