Wednesday, March 27, 2013

BUTIAMA WATAKIWA KUITUNZA MIRADI YA JK

Story ya Ahmad Nandonde,BUTIHAMA.

Wito umetolewa kwa wananchi waishio katika halmashauri ya musoma vijijini iliyopo katika wilaya mpya ya Butiama kuitunza na kuilinda miradi mbali mbali iliyotekelezwa na serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na rais jakaya mrisho kikwete.
Wito huo umetolewa leo na afisa mipango wa halmashauri ya wilaya bw. mkama rugina alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliokuwa katika ziara ya ukaguzi wa miradi iliyotekelezwa na serikali wilayani humo.
BW. Mkama amesema kuwa suala la kulinda na kuithamini miradi hiyo ni jukumu lao wenyewe na hii nikutokana na miradi hiyo kujengwa kupitia fedha zao wenyewe zinazotokana na ulipaji kodi zinazopatikana kwaajili ya maendeleo ya halmashauri.
Miongoni mwa miradi hiyo ni ufugaji wa kondoo katika kata ya bwiregi chini ya kikundi cha tudumishe,mradi wa misitu, shule sekondari ya kisasa kwaajili ya masomo ya sayansi kwa wavulana,ujenzi wa barabara pamoja na wodi ya mama na mtoto itakayokuwa na chumba maalumu kwaajili ya upasuaji pindi mama anaposhindwa kujifungua katika njia ya kawaida.
Hata hivyo Bw. mkama ameelezea baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo katika kutekelezaji wa miradi hiyo amesema kuwa ni kuchelewa kukamilika kwa mradi kwa muda muafaka kutokana na upungufu wa fedha hali inayopelekea kuchelewesha kukamilisha mradi kwa mfano ujenzi wa wodi ya mama na mtoto uliochukua takriban miaka mitatu hadi kukamilika kwake.

No comments: