Monday, January 7, 2013

WANANCHI WATAKIWA KUJIUNGA NA 'SACOSS" IFIKAPO MARCH

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA

WANANCHI WA KATA YA KIGERA WILAYANI MUSOMA MKOANI MARA WANATAKIWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII NA VYAMA VYA USHIRIKA VYA KUWEKA NA KUKOPA IFIKAPO MACHI 30 MWAKA HUU
HAYO YAMESEMA NA MTENDAJI WA KATA YA KIGERA MADURU KITULA KUWA KUTOKANA NA SEMINA MBALIMBALI ZINAZOTOLEWA WILAYANI HAPA WANANCHI WANAPASWA KUJIUNGA NA HUDUMA YA AFYA KUPITIA MIFUKO YA JAMII CHF NA NHF
AMESEMA KUWA HUDUMA ZA MATIBABU YA CHF NI YA BABA, MAMA NA WATOTO WENYE UMRI CHINI YA MIAKA 18 AU MTU YEYOTE MWENYE ZAIDI YA UMRI WA MIAKA 18 NA TAASISI KAMA SHULE, WANAUSHIRIKA NA VIKUNDI VYA UZALISHAJI
AKIFAFANUA KUHUSU MFUKO WA AFYA YA JAMII MTENDAJI HUYO AMESEMA NI MPANGO WA UCHANGIAJI HUDUMA YA MATIBABAU YA KAYA AU FAMILIA KABLA YA KUUGUA NA KWAMBA KAYA AU FAMILIA INAPATA HUDUMA YA MATIBABU KWA KIPINDI CHA MWAKA MZIMA BILA NYONGEZA YA MALIPO ZIADA
MADURU KITULA AMESEMA INAWEZEKANA KUJIUNGA MTU BINAFSI AU VIKUNDI NA KUPATIWA KADI YA UANACHAMA AMBAPO KILA KAYA ITACHANGIA KIASI KILICHOKUBALIWA CHA SHILINGI ELFU KWA MWAKA
AIDHA AMESEMA MALENGO YA KAUNZISHWA KWA MFUKO HUO NI KUIWEZEWSHA JAMII KUMILIKI HUDUMA ZA AFYA ZINAZOWAHUSU KATIKA MAENEO WANAYOISHI NA KUCHANGIA KWA HALI NA MALI HUDUMA ZA AFYA ZINAZOHUSU WANANCHI KATIKA NGAZI YA KIJIJI, KATA, TARAFA HADI WILAYA
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,


No comments: