Monday, January 7, 2013

WAFANYABIASHARA TARIME WAMCHIMBA MKWARA MKUU WA WILAYA

Story ya Ahmad Nandonde, TARIME

SIKU CHACHE BAADA YA SERIKALI WILAYANI TARIME MKOANI MARA, KUKAMATA MALORI YENYE SHEHENA YA MAHINDI KUTOKA SIRARI, UMOJA WA WAFANYABIASHARA, WAKULIMA NA WASAFIRISHAJI TARIME, UMETOA SIKU MBILI KWA MKUU WA WILAYA HIYO, JOHN HENJEWELE KUYAACHIA MARA MOJA MAGARI HAYO.
UMOJA HUO WA MUDA UMESEMA, KITENDO CHA MKUU HUYO WA WILAYA KUNG’ANG’ANIA SHEHENA HIYO NI UONEVU USIOVUMILIKA, HIVYO IWAPO HATAYAACHIA MAGARI HAYO WATAITISHA MAANDAMANO MAKUBWA KUPINGA KILICHODAIWA UNYANYASAJI.
KATIBU WA UMOJA HUO, CHACHA HECHE, ALITOA KAULI HIYO JANA ALIPOZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSIANA NA KUZUILIWA KWA SHEHENA HIYO BILA SABABU ZA MSINGI.
DESEMBA 29 MWAKA JANA, INADAIWA KARIBU MALORI 20 YENYE SHEHENA YA MAHINDI, YALIKAMATWA MAENEO YA TARIME NA MENGINE WILAYANI RORYA KWA MADAI YAMEBEBA MAHINDI YENYE SUMU KUTOKA NCHI JIRANI YA KENYA, JAMBO AMBALO LIMEKANUSHWA NA WAFANYABIASHARA HAO.
KWA HALI HIYO, HECHE ALIMTAKA DC HUYO KUTAYARISHA ASKARI POLISI NA SILAHA ZA KUTOSHA KWA AJILI YA KUDHIBITI UMMA WA SIRARI NA TARIME UTAKAOJITOKEZA KUANDAMANA KUPINGA KITENDO HICHO.
KWA UPANDE WAKE, MBUNGE WA VITI MAALUMU, ESTER MATIKO, ALIMTAKA WAZIRI WA CHAKULA, KILIMO NA USHIRIKA, CHRISTOPHER CHIZA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA HAO WANATENDEWA HAKI NA SI KUNYANYASWA.

No comments: