Monday, January 7, 2013

45 WAHUDHURIA MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINISIA

  • Story ya Ahmad Nandonde,MUSOMA.
    JUMLA YA WASHIRIKI WAPATAO 45 LEO WAMEHUDHURIA WARSHA YA MAFUNZO MAALUMU KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KWA WATOTO WA KIKE, KUKOMESHA NDOA ZA UTOTONI NA ELIMU YA UJASILIAMALI INAYOENDESHWA NA CHAMA CHA UZAZI NA MALEZI BORA TANZANIA UMATI.
    AKIZUNGUIMZA WAKATI WA UFUNGUZI WA WARSHA HIYO KWA NIABA YA MGENI RASMI AMBAYE PIA NI MGANGA MKUU WA WILAYA DK.GECHWERE MAKENGE, BW. MRATIBU WA SHUGHULI ZA BIMA YA AFYA DK.GIDEON MKINGIRA AMEWAASA WASHIRIKI HAO KUWA TAYARI KUWAFIKIISHIA UJUMBE WENZAO WALIOPO MAJUMBANI ELIMU WANAYOIPATA KWA NADHARIA NA KWA VITENDO ILI IWEZE KUWAPA TIJA KATIKA JAMII ZAO NA TANZANIA KWA UJUMLA.
    AIDHA DK. MKINGIRA AMESEMA KUFUARIA MKOA WA MARA KUKABILIWA NA VITENDO VYA UNYANYASAJI WA KIJINSIA KAMA VILE UKEKETAJI KWA WANAWAKE PAMOJA NA UBAKAJI MIMBA, WATOTO WA MITAANI NA HATA NDOA ZA UTOTONI AMEWATAJA WASHIRIKI HAO KUPAMBANA VYOVYOTE IWEZEKANAVYO ILI KUONDOKANA NA CHANGAMOTO HIZO.
    AWALI MRATIBU MRADI KATIKA MRADI WA UTETEZI WA WASICHANA KUTOKA CHAMA CHA UZAZI NA MALEZI (UMATI) BW. BARNABA RICHARD UTEGE AMEZITAJA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI KUWA NI KUTOPATA USHIRIKIANO WA KIUSHAIDI TOKA KWA WASICHANA WANAONYANYASWA KIJINSIA PINDI KESI ZINAPOFULIWA DHIDI YA WANAOWANYANYASA.
    AIDHA BW. UTEGE AMEITAKA SERIKALI, ASASI ZA KIRAI MASHIRIKA YA DINI NA WADAU MBALI MBALI KUFANYA JITIHADA ZA PAMOJA NA KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA ILI KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE.
    WARSHA HIYO YA SIKU SITA ILIYOANZA LEO INAFANYIKA KATIKA UKUMBI WA ANGLIKANA ULIOPO MUSOMA MJINI INATARAJIWA KUMALIZIKA SIKU YA JUMAMOSI TAR 13 MWEZI HUU.

    No comments: