Monday, January 7, 2013

NHC LAJENGA VYOO 14 KWENYE SHULE ALIYOSOMA MWL. NYERERE

Story ya Ahmad Nandonde, Musoma.
SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA NHC LIMEJENGA MATUNDU 14 VYOO KATIKA SHULE YA MSINGI MWISENGE ALIYOSOMA BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARANGE NYERERE IKIWA NI SEHEMU YA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA SHIRIKA HILO.
KATIKA HOTUBA YAKE YA UZINDUZI WA JENGO HILO ULIOFANYIKA SHULENI HAPO, MENEJA WA
HUDUMA KWA JAMII WA SHIRIKA HILO MUUNGANO SAGUYA AMESEMA KUWA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA KWA KUTAMBUA WAJIBU WAKE KWA JAMII LINAYO SERA YA KUSAIDIA MAENDELEO YA JAMII KATIKA NYANJA MBALIMBALI.

AMESEMA LICHA YA KUWEPO KWA CHANGAMOTO MBALIMBALI KATIKA SHULE HIYO YENYE HISTORIA KUBWA KATIKA TAIFA LA TANZANIA WAMEJARIBU KUPUNGUZA CHANGAMOTO HIZO KWA KUBORESHA MIUNDOMBINU NA VYOO AMBAVYO IMEGHARIMU KIASI CHA SHILINGI MILLIONI 16 ILI KUVIWEKA KATIKA HALI YA KURIDHISHA.
AMESEMA NHC ILI KUHAKIKISHA WANAFUNZI WANAPATA ELIMU BORA HAWANABUDI KUPATA MAHALA PAZURI PA KUJISITIRI HALI ILIYOPELEKEA KUTOA MSAADA HUO KWA KUTENGENEZA VYOO VYA KISASA SHULENI HAPO.
KATIKA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA MENEJA WA NHC MKOA WA MARA JACTON MATOGO KUHUSU UJENZI HUO AMESEMA KUWA UJENZI ULIANZA TANGU JULAI 2012 NA KUKAMILIKA OCTOBA 2012 IKIWA NA MATUNDU SABA KWA WASICHANA NA MATUNDU SABA KWA WAVULANA.
SAGUYA AMESEMA MRADI WA CHOO CHA WANAFUNZI KATIKA SHULE HIYO ULIIBULIWA NA UONGOZI WA SHULE BAADA YA KUTATHMINI MAHITAJI YA HARAKA NA KUTIMIZA SEHEMU YA MIRADI YA HUDUMA KWA JAMII INAYOTOLEWA NA SHIRIKA HILO.

No comments: