Saturday, January 12, 2013

MWANAMKE AUA MTOTO WAKE, AMCHUNA NGOZI , ANYOFOA SEHEMU ZA MWILI

Story ya Ahmad Nandonde, TARIME

MWANAMKE mmoja mkazi wa mtaa wa Mwangaza Bi Prisca Mwita (22) anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kumuawa kikatili mtoto wake mwenye umri wa miezi kumi na moja kisha kumchuna ngozi katika baadhi ya sehemu yake ya mwili na kunyofoa baadhi ya viungo vyake vya mwili.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu Kamanda wa polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya kamishina msaidizi Justus Kamugisha, amesema kuwa mtoto huyo Happy Anthony aliokotwa januari 11 majira ya saa mbili asbuhi katika mtaa wa huo wa Mwangaza kata ya misangura wilayani Tarime.
Amesema kuwa kuokotwa kwa mtoto huyo kunafuatia taarifa ambazo zilimfikia mwenyekiti wa Kitongoji hicho kuwapo kwa mtoto huyo katika eneo hilo.
Kamanda Kamugisha amesema kuwa baada ya mtoto huyo kuokotwa akiwa amekufa alikutwa amekatwa sikio la kushoto,kuondolewa nyusi jicho za kushoto,nywele pamoja na kuchunwa ngozi katika kichwa chake upande wa kushoto.
Hata hivyo kamanda Kamugisha,amesema tayari mama wa mtoto huyo amekamatwa kwa mahojiano ingawa amekataa kutenda kosa hilo na tayari mwili wa mtoto huyo umefanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu na jamaa kwaajili ya uchunguzi.


No comments: