WANANCHI wa maeneo ya Majengo na Kipondoda wilayani Manyoni Mkoani Singida wanatarajia kufanya maandamano makubwa hivi karibuni kupinga hatua ya uongozi wa wilaya kuwanyang’anya maeneo yao na kuyauza kwa watu wengine huku wenye maeneo wakiachwa bila kupewa fidia yeyote.
Mwenyekiti anayeratibu maandamano hayo, Ufinyu Cheliga akizungumza na Tanzania Daima katka mahojina maalum alisema wanatarajia kufanya maandamano makubwa ya Amani kupinga kunyang’anywa maeneo yao.
Kwa mujibu wa mratibu huyo alisema maeneo hayo wanayamiliki kihalali na wanatarajia kuwakilisha kilio chao hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Mratibu huyo pia alieleza kuwa wanakusudia kumwomba mkuu wa mkoa awafukuze kazi Mkurugenzi wa wilaya,Afisa Ardhi na mwenyekiti wa Halmashauri kwa sababu wao ndiyo chanzo ga migogoro.
“Hatuna haja tena ya kuendelea kumwambia mkuu wa Wilaya ama mkurugenzi sasa maamuzi yetu ni kuonana na mkuu wa Mkoa na ikishindikana tutaonana na Waziri wa ardhi Nyumba na Maendeleo na Makazi Prof. Anne Tibaijuka na ikishindikana kwake tutapanda hadi kwa Waziri Mkuu na ikishindikana hapo tutamwoma Rais na kama hatutapama majibu tutajua ni jinsi gani ya kuiadhibu serikali…..
“Hatuwezi kuendelea kuteseka wakati ardhi ni yetu na tunayo lakini wapo watu ambao wao ndiyo wanajifanya miungu watu kamwe hatuwezi kukubaliana na jambo hili na ikumbukwe mwaka 2015 siyo mbali kwani mshahara wa dhambi ni mauti” alisema .
Pia alibainisha kuwa wananchi kwa sasa wamekosa imani na mkuu wa wilaya kwani hiyo kutokana na kushindwa kushghulikia migogoro ya ardhi mapema.
Alipotafutwa Mkurugenzi wa wilaya ya manyoni Fotunata Marya kwa njia ya simu yake ya kiganjani hakuweza kupokea simu kwani ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
Katika juhudi za kuhakikisha zinapatikana taarifa kutoka kwa walalamikiwa zilifanyika na kumpata Ofisa Ardhi wa Wilaya ya Manyoni, Leonard Msafiri ambaye alisema kuwa mgogoro hupo lakini unatokana na kuwepo kwa baadhi ya wanasiasa ambao wanachochea tatizo hilo.
Alisema kuwa kutokana na kukua kwa kasi mji wa singida na watu kuendelea na ujenzi holele halmashauri kwa kushirikiana baraza la madiwani waliweka mpango mkakati wa kuanzisha mradi wa upimaji wa viwanja.
“Pamoja na kuwa hatukuwa na fedha lakini kwa kushirikiana na baraza la madiwani pamoja na wananchi ambao wanamiliki mashamba na maeneo makubwa tulikubaliana kupima maeneo ili kuondokana na ujenzi holele…….
“Baadaye tuliomba mkopo wa sh.mil 77 kwa ajili ya upimaji na makubaliano yakawa kila mwenye shamba ama kiwanja kikubwa atapimiwa atapewa viwanja viwili kwanza na vitakavyo baki atauziwa kwa nusu bei tofauti na mtu ambaye ni mgeni na hakuwa na shamba jambo ambalo lilikubaiwa na kamati zote” alieleza msafiri.
Alisema kuwa viwanja vilivyo pimwa ni 740 kutokana na mashamba ya watu na viwanja hivyo vinauzwa kati y ash.laki 270000 na 340,000 na vikubwa vinauzwa katika ya mil.1.6.
Pamoja na wananchi hao kupewa viwajia hivyo lakini wale wote ambao walikuwa na mashamba watalipwa fidia zao kulingana na tathimini iliyofanyika nivyo hakuna mtu ambaye atadhurumiwa.
Naye mkuu wa Wilaya ya Manyoni Fatma Toufiq akiongea katika mahojiano maalum alikiri kuwepo kwa migogoro ya Ardhi na tayari kero zote zimeshafika mezani kwake anazishughulikia na kuhakikisha anazimaliza.
No comments:
Post a Comment