Saturday, January 12, 2013

MUME AMTOA JICHO MKE WAKE

Story ya Ahmad Nandonde, BUTIMA
MATUKIO ya Ukatili wa Kijinsia kwa Wanawake bado yanaendelea kutokea katika Jamii ya mkoani Mara baada ya Mwanamke mmoja Bi Christina Fabiani mwenye umri wa miaka 27 kupigwa na mtu aliyemtaja ni mume wake hadi kumtoa jicho la kulia.
Akizungumza waandishi wa habari akiwa na baba ake mzazi Fabian Marengo,amesema mme wake huyo ambaye amemtaja kwa jina la Magige Kisyeri alimpiga kwa kutumia fimbo,mijaredi na marungu kisha kumkimbiza hospitalini kwaajili ya matibabu.
Amesema tukio hilo ametokea Januari Mosi mwaka huu baada ya kuondoka nyumbani kwake anapoishi katika Kijiji cha Baranga Butiama kwa lengo la kwenda kumuogesha mama mkwe wake anayeishi katika kijiji hicho ambaye ni mgonjwa na aliporudi ndipo alipokutana na adha ya kipigo kutoka kwa mume wake huyo.
Mwanamke huyo amesema baada ya kurejea nyumbani majira ya jioni ya siku hiyo alimkuta mume wake akiwa amesharudi nyumbani na kumhoji sababu ambazo zimefanya kwenda ukweni bila ridhaa yake na baada ya kutoa majibu hayo ndipo alipoanza kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake.

Hata hivyo mwanamke huyo amesema baada ya kuona amempasua jicho hilo alimkimbiza hospitali ya mkoa kabla ya kwenda polisi kuchukua fomu namba tatu kwa kutoa taarifa za uongo kuwa majeraha hayo ameyapata baada ya kuvamiwa na majambazi.
Kwa upande wa baba mzazi wa Mwanamke huyo Bw Fabiani Marengo,amesema alipata taarifa kutoka kwa majirani juu ya tukio la kupigwa kwa mtoto wake hivyo kuomba serikali kupitia jeshi la polisi kumsaka mtuhumiwa huyo ambaye alitoweka na kumtelekeza mkewe hospitalini.


Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi,mwandamizi Absalom Mwakyoma,amethibitisha kuripotiwa kwa tukio hilo katika kituo kikuu cha polisi na kwamba juhudi za kumtafuta mtuhumiwa ili afikishwe katika vyombo vya sheria bado zinaendelea

No comments: