Friday, January 11, 2013

KIWANDA CHA MAZIWA MARA CHAPATA HASARA YA M 8

Story ya Ahmad Nandonde , MUSOMA 
KIWANDA CHA MAZIWA CHA MARA (MARA MILK) MUSOMA KIMEPATA HASARA ZAIDI YA SHILLINGI MILIONI 8 ILIYOSABABISHWA NA ITILAFU YA UMEME ILIYOTOKEA JANUARI 9 MWAKA HUU.
AKIONGEA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE LEO HII MKURUGENZI MTENDAJI WA KIWANDA HICHO JAMES MATHAYO AMESEMA KUWA KIWANDA HICHO KIMESIMAMA KWA MUDA WA SIKU MBILI KUTOKANA NA UHARIBIFU WA BAADHI YA VIFAA VYA KIWANDA HICHO.
AMESEMA KUWA BAADA YA ITILAFU YA UMEME KUTOKEA VIFAA VIWILI VYA MOTO VILIUNGUA AMBAVYO ALIVITAJA KUWA NI HEATER ELEMENT YENYE GHARAMA YA SHILINGI 3.6 NA PAMPU YAKUPOOZA MAJI CHILLER MACHINE YENYE THAMANI YA SHILINGI MILLIONI 1.2. NA KWAMBA VINAPATIKANA NCHI JIRANI YA KENYA NAITAWALAZIMU KUVINUNUA.
NAYE KAIMU MENEJA WA KIWANDA HICHO AMBAYE PIA NI PLAN ENGENEER WA TANESCO MKOA WA MARA AMEKIRI KUWEPO KWA TATIZO HILO NA AMESEMA KUWA WANATAMBUA MCHANGO WA KIWANDA HICHO KWA SHIRIKA LA UMEME MKOANI HUMO NA WAMEOMBA RADHI KWA USUMBUFU HUO NA KWAMBA WANAENDELEA KULITAFUTIA UFUMBUZI.
AMESEMA KUWA ITILAFU HIYO IMETOKEA KUTOKANA NA KUANGUKA KWA TRANSFOMA INAYOHUDUMIA KIWANDA HICHO NA TAYARI WAMEKWISHA BADILISHA NA KUWEKA TRANSFOMA NYINGINE.
KIWANDA CHA MAZIWA MARA MILK KINAZALISHA MAZIWA YA MTINDI, YOGATI, NA MAJI YA KUNYWA AINA YA SUPER WATER.

No comments: