Thursday, January 10, 2013

DIWANI WA CCM AKAMATWA KUHUSIANA NA MAUAJI YA MUSOMA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA.
JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA WATU KUMI NA TANO AKIWEMO DIWANI MMOJA WA CCM KATIKA KATA YA MUGANGO WILAYA YA BUTIAMA KUHUSIANA NA MAUAJI YA KINYAMA NA KIKATILI AMBAYO YAMEIBUKA HIVI KARIBUNI MKOANI MARA HASA KATIKA WILAYA ZA BUTIAMA NA MUSOMA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI SACP ABSALOM MWAKYOMA,AMEWAMBIA WAANDISHI WA HABARI MJINI MUSOMA KUWA WATU HAO WAMEKAMATWA KATIKA OPARESHENI KUBWA INAYOENDESHWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MARA NA MAKAO MAKUU YA JESHI HILO IKIONGOZWA MKUU WA OPARESHENI SAIMON SIRO.
AMEMTAJA DIWANI NI BW WANDWI MAGURU WA KATA YA MUGANGO AMBAYE AMEKAMATWA JANA AKIWA NI MIONGONI MWA WATU KUMI NA TANO AMBAO TAYARI WAMEKAMATWA KUHUSIANA NA MATUKIO YA KUUAWA KWA WATU KWA KUCHINJWA NA WAUAJI KUONDOKA NA BAADHI YA VIUNGO VYAO.
SIKU MBILI ZILIZOPITA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI,IGP SAID MWEMA,ALIIAMBIA RADIO ONE STREO KUWA JESHI HILO LIMETUMA TIMU MAALUM YA ASKARI WAKE AMBAO WATAONGEZA NGUVU KATIKA OPARESHENI KUBWA YA KUWASAKA WATU WANATUHUMIWA KWA MAUAJI YA KINYAMA NA KIKATILI YANAYOENDELEA MKOANI MARA. 
IGP MWEMA AMESEMA OPARESHENI HIYO KUBWA INAFANYIKA KATIKA MAENEO MBALIMBALI MKOANI MARA HASA KATIKA WILAYA YALIPOTOKEA MAUAJI HAYO HUKU AKISEMA HATUA HIYO INAFANYIKA BAADA KUKAMILIKA KWA KAZI YA UKUSANYAJI WA TAARIFA MUHIMU AMBAYO IMEFANYWA NA TIMU YA WATALAAM JESHI HILO KUTOKA MAKAO MAKUU KWA KUSHIRIKIANA UONGOZI WA POLISI MKOANI MARA.
KWA SABABU HIYO IGP MWEMA AMEWAOMBA WANANCHI,VIONGOZI WA VIJIJI,MITAA NA WATU WENYE TAARIFA KUHAKIKISHA KUWA WANATOA USHIRIKIANO WA KUTOSHA AMBAO UTAKAO WEZESHA KUKAMATWA KWA WATUMIWA WOTE ILI WAWEZE KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.

No comments: