Wednesday, January 2, 2013

MWANAMKE ALIYE UA MTOTO WAKE AKAMATWA , MARA

Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA
JESHI LA POLISI MKOANI MARA LINAMSHIKILIA MWANAMKE MMOJA KWA TUHUMA YA KUUA MTOTO WAKE KWA KIPIGO, IKIWA NI PAMOJA NA KUMCHOMA MOTO KWA KUTUMIA CHUMA KATIKA KICHWANI NA MIKONONI.
KAMANDA WA POLISI MKOANI MARA, ABSALOM MWAKYOMA, AMESEMA KUWA TUKIO HILO LILITOKEA MNAMO DESEMBA 30, MWAKA JANA, MAJIRA YA USIKU KATIKA KIJIJI CHA KWITETE, WILAYANI SERENGETI.
KAMANDA MWAKYOMA AMEMTAJA MWANAMKE ANAYESHIKILIWA KUWA NI GHATI RANGE (30), MKAZI WA KIJIJI HICHO NA KWAMBA ANATUHUMIWA KUMUUA MTOTO WAKE, RYOBA JUMA (3).
AMESEMA MWANAMKE HUYO AMEMPIGA MTOTO WAKE SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KWA KUTUMIA FIMBO NA KISHA AKAMCHOMA NA CHUMA CHA MOTO KICHWANI NA MIKOANI, BAADA YA MTOTO HUYO KUKOMBA MBOGA CHUNGUNI NA KUCHEZEA KINYESI.
AMESEMA BAADA YA KUMPA ADHABU HIYO ALIMFUNGIA NDANI YA NYUMBA KWA ZAIDI YA WIKI MOJA BILA YA KUMPATIA MATIBABU YOYOTE HALI ILIYOPELEKEA MTOTO HUYO KUPOTEZA MAISHA NA KWAMBA MWANAMKE HUYO ATAFIKISHWA MAHAKAMANI WAKATI WOWOTE KUJIBU TUHUMA ZA MAUAJI.
AMESEMA KUWA BAADA YA MTOTO HUYO KUWA AMEFARIKI MWANAMKE HUYO ALIANZA KUANGUA KILIO HALI ILIYOPELEKEA MAJIRANI KUFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO NA NDIPO MWANAMKE HUYO AKAKIRI KWAMBA ALIMPATIA ADHABU HIYO.

No comments: