Wednesday, January 2, 2013

BUNDA WAPUNGUZA VIFO VYA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

Story ya Ahmad Nandonde, BUNDA
WILAYA YA BUNDA MKOANI MARA IMEPUNGUZA VIFO VYA WATOTO CHINI YA UMRI WA MIAKA MITANO KWA KIWANGO CHA ASILIMIA 16 KWA MIAKA MINNE ILIYOPITA KUTOKANA NA MWITIKIO WA WAZAZI KUWAPELEKA WATOTO CHANJO.

KIWANGO HICHO NI KUTOKA ASIMILIA 77 MWAKA 2008 HADI KUFIKIA ASILIMIA 93 MWAKA 2012 AMBAPO KATIKA MIAKA MIWILI IJAYO WILAYA YA BUNDA INALENGA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO KWA ASILIMIA 96.

HAYO YAMEELEZWA NA MGANGA MKUU WA WILAYA YA BUNDA DK RAINER KAPINGA WAKATI WA UZINDUZI WA CHANJO MPYA YA WATOTO DHIDI YA MAGONJWA YA NIMONIA NA ROTA KUHARA ILIYOFANYIKA WILAYANI BUNDA.

DK KAPINGA AMESEMA KUWA CHANJO YA NIMONIA INAYOJULIKANA KITAALAM KAMA PCV 13 INALENGA KUWAKINGA WATOTO KUTOKANA NA MAGONJWA YA VICHOMI AMBAPO ROTA VIRUS INAWAKINGA NA KUHARA.

AKIZUNDUA CHANJO HIZO KATIKA ZAHANATI YA BUNDA, MKUU WA WILAYA YA BUNDA BW JOSHUA MIRUMBE, AMEWAHIMIZA WAZAZI NA WALEZI KUHAKIKISHA KUWA WANAWAPELEKA WATOTO WAO KUPATA CHANJO HIZO.

AMESEMA SERIKALI INATUMIA FEDHA NYINGI KUGHARAMIA CHANJO HIZO AMBAPO GHARAMA YA MTOTO MMOJA NI SHILINGI 51,218.85 NA KWAMBA GHARAMA HIZO ZILIZOTAKIWA KUTOLEWA NA MZAZI ZIMEFADHALIWA NA SERIKALI KWAKUSHIRIKIANA NA WAHISANI WENGINE.

No comments: