Thursday, January 17, 2013

MWALIMU MWAKASEGE LEO HII KATIKA FACEBOOK


Shalom!!
Je, unajua Yesu jina lake jingine anaitwa nani?
Mzee Yusufu alipokuwa anaelezwa juu ya kuzaliwa ka Yesu na malaika kwa njia ya ndoto aliambiwa juu ya majina mawili ya mtoto huyo na kilichobebwa na majina hayo.
Jina la kwanza aliambiwa katika Mathayo 1:21 ya kuwa: "nawe utamwita jina lake Yesu, maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao".
Jina la Pili aliambiwa katika Mathayo 1:23 ya kuwa: " Nao watamwita jina lake Imanueli,yaani Mungu pamoja nasi".
Unadaka hili moyoni mwako? Ndani ya jina la Yesu kuna kukombolewa toka dhambini. Je kuna dhambi inakusumbua,liitie jina la Yesu uone jinsi nguvu za Mungu toka ndani ya jina hili zitakavyokusaidia.
Unajisikia mpweke?Unajisikia kuchukiwa?Unajisikia kukataliwa?kumbuka ndani ya jina la Yesu kuna nguvu za Imanueli, yaani uwepo wa Mungu ukijifunua kwako na kwa upande wako. Daka na hili pia moyoni mwako!
Mungu awatunze na kuwabariki.
Like ·  ·  · 12 hours ago · 

No comments: