Wednesday, January 16, 2013

HABARI MPYAAAAAAAAAA !!!!!!!!! AJALI YA DALADALA USIKU HUU MBEZI MSIGANI , DAR ES SALAAM
Abiria ambao walikuwa wamepanda gari aina ya Coaster T723 ambayo ni daladal inayofanya safari yake kutoka Malamba Mawili hadi Mbezi mwisho wamenusurika kufa baada ya gari hiyo kushindwa kupanda mlima na kurudi kinyume nyume na kisha kupinduka.
Kwa mujibu ya mashuhuda ambao walikuwapo eneo la tukio wanasema kuwa ajali hiyo imetokea majira ya saa moja usiku huu maeneo ya Msigani CCM na kusababisha mtafaluku mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo na abiria waliokuwepo kwenye gari hiyo.
Mashuhuda hao wanasema kuwa dereva alipokuwa anapandisha kilima hicho alikuwa anajaribu kuingiza gia ndipo zilipokataa na kusababisha gari hiyo kukataa kupanda mlima na kurudi kinyume nyume na kisha kupinduka, na kwa taarifa nilizopata kuwa dereva wa gari hiyo aliyojulikana kwa jina moja la Mgosi amekimbia baada ya ajali hiyo kutokea.
Na taarifa niliyoipata sehemu hiyo ya tukio inasemekana konda wa gari hiyo ambae na yeye amejulikana kwa jina moja la Toll amechubuka magotini na sijapata taarifa ya kufa mtu, taarifa zaidi tutaendelea kujuzana (PICHA NA FATUMA MAUMBA) KUPITIA FACEBOOK .

No comments: