Tuesday, January 15, 2013

WWATAKAO KIUKA BEI ELEKEZI MUSOMA KUKIONA


Story ya Ahmad Nandonde, MUSOMA
Serikali Mkoani Mara Imesema Haitasita Kumchukulia Hatua Mfanyabishara Yoyote Aliyepewa Kibali Cha Kufuata Mahindi Kutoka Katika Ghala Serikali Na Kuuza Kwa Bei Elekezi Ya Shilingi Mia Saba.
Kauli Hiyo Ya Serikali Imekuja Kufuatia Malalamiko Ya Wananchi Wa Kata Mbalimbali Katika Manispaa Ya Musoma Ambao Wamesema Kuwa Wanauziwa Mahindi Kwa Bei Ya Shilingi Mia Saba Na Hamsini Hadi Mia Tisa.
Akizungumza Na Radio Victoria Fm Ofisini Kwake Hii Leo Afisa Biashara Wa Manspaa Bw Victor Rulegea Amekiri Kuwepo Kwa Wafanyabiashara Hao Wanaokwenda Kinyume Na Maelekezo Ya Serikali Ambapo Ofisi Yake Kwa Kushirikiana Na Ofisi Ya Afisa Afya Wa Manispaa Hiyo Wameanza Msako Maalumu Wa Kuwabaini Wale Wote Wanaokwenda Kinyume Na Agizo La Serikali.
Aidha Victor Amesema Kuwa Kikao Cha Kamati Ya Maafa Chini Ya Mwenyekiti Wa Kamati Hiyo Ambaye Ni Mkuu Wa Wilaya Musoma Bw Jacksoni Msom Kiliagiza Mahindi Hayo Yauzwe Kwa Shilingi Mia Saba Kwa Kilo Na Unga Wa Sembe Kuuzwa Kwa Kilo Shilingi Mia Saba Hamsini Hadi Mia Tisa Lakini Hii Leo Katika Msako Uliofanyika Wamebaini Kuwa Kuna Wafanya Biashara Ambao Wamekuwa Wakiwauzia Wananchi Kwa Bei Ya Shilingi Mia Tisa Hadi Mia Tisa Hamsini Ambapo Wamechukua Hatua Dhidi Ya Wale Wote Waliokiuka Maagizo Ya Kamati Ya Maafa Ikiwa Ni Pamoja Na Kuwaamuru Kuuza Kwa Bei Iliyopangwa
Hata Hivyo Amewaomba Wananchi Kutoa Taarifa Kwa Wenyeviti Wa Serikali Za Mitaa Yao, Ikiwa Watauziwa Mahindi Ya Serikali Ya Bei Nafuu Kwa Bei Tofauti Na Shilingi Mia Saba.

No comments: