Wednesday, December 12, 2012

WANANCHI TUMIENI VITUO VYA UTAFITI


Wananchi wametakiwa kutumia kituo cha utafiti cha Naliendele ili waweze kunufaika na tafiti zinazofanywa na kituo hiko.
Wito huo umetolewa hii leo na mkurugenzi wa kituo hiko Dk Wlly Kafiriti alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Naliendele
Dk Kafiriti amesema kituo hiko kipo kwa ajili ya kuwasaidia wakulima wote Nchini, lakini hususani wakazi wa kusini na hivyo ni vema wananchi hao wakatumia kituo hiko vizuri.
Amesema kuwa inasikitisha kupokea simu za wakulima kutoka mikoa ya kaskazini wakiulizia kuhusu matumizi ya mbegu mbalimbali huku wananchi wenyewe wa mtwara wakishindwa kufanya hivyo.
Amesema kuwa kituo chake kipo wazi kupokea mahitaji ya mkuliam yeyote anayehitaji mbegu zilizofanyiwa tafiti na zenye ubora kutoka katika kituo hiko.

Story ya Idrisa Bandali , MTWARA

No comments: