Sunday, December 9, 2012

HOSPITALI YA BUNDA YAKABILIWA NA CHANGAMOTO KIBAO

Story ya Ahmad Nandonde, BUNDA
Upungufu Mkubwa Wa Dawa Na Vifaa Tiba Pamoja Na Huduma Muhimu Ya Maji Na Nishati Ya Umeme Ni Miongoni Mwa Matatizo Makubwa Yanayoikabili Hospitali Teuli Ya Wilaya Ya Bunda Mkoani Mara.

Hatua Hiyo Imesababisha Hospitali Hiyo Kushindwa Kutoa Huduma Nzuri Kwa Wananchi Wa Wilaya Hiyo Ya Bunda Na Vijiji Jirani Vya Wilaya Za Serengeti Mkoani Mara Na Busega Mkoani Simiyu.
Taarifa Hiyo Imetolewa Na Uongozi Wa Hospitali Hiyo Ya Bunda Ddh,Wakati Wa Ziara Ya Kamati Ya Madiwani Ya Fedha,Uongozi Na Mipango Ya Halmashauri Ya Wilaya Ya Bunda.
Mganga Mfawidhi Wa Hospitali Hiyo Dk William Krekamoo Amesema Tatizo La Ukosefu Wa Dawa Pamoja Na Kuchangiwa Bohari Ya Kuu Ya Dawa Msd Lakini Ukosefu Wa Fedha Ni Moja Changamoto Kubwa Unaikabili Hospitali Hiyo Kwa Vile Imekuwa Ikitoa Huduma Bure Kwa Aslimia 86 Ya Wagonjwa Wa Makundi Maalum Jambo Linalochangia Upungufu Wa Mapato.
Kwa Upande Wao Baadhi Ya Wajumbe Wa Kamati Hiyo Ya Fedha,Uongozi Na Mipango Katika Halmashauri Ya Bunda,Wakizungumza Baada Ya Kutembelea Na Kufanya Ukaguzi Katika Hospitali Hiyo,Wamekiri Kuwa Hospitali
Hiyo Licha Ya Kukabiliwa Na Upungufu Mkubwa Wa Dawa,Vifaa Tiba Na Watumishi Lakini Pia Wamebaini Ukosefu Wa Huduma Ya Maji Na Nishati Ni Miongoni MwaMatatizo Makubwa Yanayopaswa Kushughulikiwa Mapema Ili Kuboresha Huduma Za Hospitali Hiyo.
Hivi Karibuni Uongozi Wa Hospitali Hiyo Ya Bunda Ddh Umetangaza Kusitisha Kutoa Huduma Za Bure Za Matibabu Kwa Kundi La Watoto Chini Ya Miaka Mitano,Wajawazito Na Wazee Kutokana Serikali Kushindwa Kuipatia Hospitali Hiyo Ruzuku Kwa Kipindi Kirefu Sasa.

No comments: