Sunday, December 16, 2012

WAKULIMA WA TUMBAKU,.. SERIKALI SIMAMIENI ZAO LETU


Story ya Ahmad Nandone, MUSOMA
WAKULIMA WA ZAO LA TUMBAKU MKOA WA MARA WAMEIOMBA SERIKALI KUSIMAMIA KIKAMILIFU UNUNUZI WA ZAO HILO ILI MKULIMA AWEZE KULIPWA KWA WAKATI LA SIVYO WATATOROSHA TUMBAKU ZAO KWENDA KUUZA NCHINI KENYA.

KAULI HIYO IMETOLEWA JANA NA WAKULIMA WA ZAO HILO KATIKA MKUTANO WA MWAKA WA WAKULIMA NA WADAU WA TUMBAKU ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA UWEKEZAJI WA MKOA HUO.

AKITOA MADA JUU YA SHERIA, KANUNI BNA TARATIBU ZA ZAO HILO NCHINI, MTEUZI WA BODI YA TUMBAKU STANLEY MNOZYA AMESEMA KUWA KILIMO CHA TUMBAKU KIMEPITISHWA RASMI MKOANI HUMO.

MNOZYA AMESEMA KUWA UTARATIBU WA UPATIKANAJI WA PEMBEJEO KWA MSIMU UJAO WA KILIMO 2013/14 UWE NDANI YA NCHI KWANI KWA KIPINDI CHOTE CHA MAJARIBIO PEMBEJEO HIZO ZILITOLEWA NA KAMPUNI YA UNUNUZI YA AOTTLILIYOKUWA INAENDESHA MAJARIBIO HAYO.

KWA UPANDE WAKE MENEJA MTENDAJI WA KAMPUNI YA ALLIANCE ONE INAYOSHUGHULIKA NA UNUNUZI WA TUMBAKU NCHINI, MARK MASON AMESEMA KUWA ZAO HILO LINA CHANGAMOTO NYINGI KATIKA UZALISHAJI WAKE.

MASON AMESEMA KUWA KITU KINGINE CHA KUZINGATIA NI KUTOKUWEPO KWA AJIRA ZA WATOTO AU AJIRA ZA LAZIMA JKWA WATAALAMU WAO WATAKUWA WANATEMBELEA MASHAMBA HAO ILI KUHAKIKISHA HILO HALIFANYIKI.

No comments: