Sunday, December 16, 2012

STORY MUHIMU KUTOKA MUSOMA MARA, HIZI HAPA


Story za Ahmad Nandonde, MUSOMA
MAHAKAMA YA WILAYA YA MUSOMA MKOANI MKOANI HAPA, IMEMHUKUMU KWENDA JELA MIAKA 7 MFANYABIASHARA MMOJA BW. MAYAI JUSTINE MKAZI WA NYAKATO MSHIKAMANO KWA KOSA LA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA.
AKISOMA HUKUMU HIYO MWISHONI MWA WIKI MAHAKAMANI HAPO,HAKIMU MFAWIDHI MWANDAMIZI WILAYA YA MUSOMA MH RICHARD MAGANGA AMESEMA BAADA YA MAHAKAMA KURIDHIKA NA USHAHIDI ALIMHUKUMU JUSTINE KUTUMIKIA KIFUNGO CHA MIAKA 7 JELA.
MBELE YA HAKIMU, MWENDESHA MASHTAKA WA SERIKALI BW JONAS KAIJAGE AMEDAI KUWA BW MAYAI JUSTINE AMBAYE NI MKAZI WA NYAKATO MSHIKAMANO MJINI MUSOMA ALIPATIKANA NA NOTI BANDIA ZA SHILINGI ELFU 50 APRIL 13 MWAKA HUU NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI MEI 17, 2012.
AKITOA HUKUMU HIYO HAKIMU MAGANGA AMESEMA KUPATIKANA NA NOTI BANDIA NI KOSA LA JINAI HIVYO ANATOA HUKUMU HIYO HILI IWE FUNDISHO KWA WAFANYABIASHARA WANAOWEZA KUFANYA KOSA KAMA HILO.
STORY NYINGINE HII HAPA 
WAFANYAKAZI NA WADAU MBALI MBALI WA RADIO VICTORIA FM LEO WANATEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MARA ILI KUJULIA HALI WAGONJWA WALIOLAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO PAMOJA NA KUWAPATIA MISAADA MBALI MBALI.
AKIZUNGUMZA NA RADIO VICTORIA FM LEO MRATIBU WA SHUGHULI HIYO BW.PATRIK DERRICK MANKALE AMESEMA ZOEZI HILO NI MOJA YA HUDUMA MUHIMU ZAKIJAMII AMBAZO KILA MWANADAMU ANATAKIWA KUZIFANYA KWANI SUALA LA KUUGUA NI SUALA LITAKALOMGUSA KILA MWANADAMU.
BW. MWANKALE AMESEMA MBALI YA UTOAJI WA MISAADA HIYO KWA WAGONJWA HOSPITALINI HAPO LAKINI PIA WATASHIRIKI KATIKA ZOEZI LA KUFANYA USAFI HOSPITALINI IKIWA NI MOJA SEHEMU AMBAYO ITAWAFANYA KUONESHA USHIRIKIANO, KUWATHAMINI NA KUWAJALI WAGONJWA WANAOPATIWA MATIBABU HOSPITALINI HAPO.
MIONGONI MWA MISAADA ITAKAYOTOLEWA KWA WAGONJWA HOSPITALINI HAPO NI PAMOJA NA SABUNI ZA KUFULIA, SABUNI ZA KUOGEA MAJI YA KUNYWA MATUNDA NA ZAWADI MBALI MBALI KWA WATOTO.
HATA HIVYO MWANKALE AMEZIOMBA BAADHI YA TAASISI, MAKUMPUNI, VIKUNDI NA MASHIRIKA YA DINI MBALI MBALI NMKOANI HAPA KUWANA MAZOEA YA KUJITOKEZA NA KUJITOLEA KUSHIRIKI KATIKA MATUKIO KAMA HAYO KWANI HUWAFANYA KUWA KARIBU NA MWEZIMUNGU NA JAMII KIUMJULA.
HII NI MARA KWANZA KWA WAFANYAKAZI NA WADAU MBALI MBALI RADIO VICTORIA KUJUMUIKA NA KUSHIRIKI KWA PAMOJA KUSHIRIKI KATIKA ZOEZI HILO LINALOINGIA KATIKA HISTORIA MPYA YA MKOA HUU WA MARA.

No comments: