Sunday, December 16, 2012

MWANAFUNZI AFARIKI CHUMBANI KWAKE, SAUT MWANZA

Mwanafunzi wa chuo kikuu cha mtakatifu Agustino SAUT Mwanza, PRAISE TOM , aliyekuwa anasoma MAHUSIANO YA UMMA, Public relations, hii leo amaekutwa amefariki akiwa kitandani kwake ndani ya hostel ya Mikumi ndani ya eneo la chuo hicho. 
Maelezo ya awali ya marafiki wa kijana huyu, wanasema usiku wa kuamkia leo alienda club kwaaajili ya utaratibu wa kuifurahia "wikiend" na aliporejea mida ya saa nane aliwaomba wenzake chumbani wasimwamshekwa kuwaalikuwaamechoka sana,  walitii agizo, ingawa kulipokucha na mida ilivyozidi kwenda rafiki yao hakuweza kuamka, na ndipo walipoona wamwamshe..... kumbe tayari alikuwa ameshalala usingizi wa moja kwa moja. 
PRAISE alikuwa mwaka wa kwanza, kwa sasa hakunastory zaidi zinazoendelea kitaa kwa kuwa wenye mamlaka (POLICE) ambao hata hivyo pamoja na kuchelewa na kuja bila hata gari kuchukua mwili huo, wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo  cha kifo cha kijana huyu.
 Dada huyu alizimia baada ya kupata taarifa hizi

Umati uliojitokeza kushuhudia tukio hilo
Gari la chuo, lilotumika kubeba mwili wa marehemu.
KIFO ni ahidi ya sisi sote kurejea kule tulikotwaaliwa, ingawa ni fumbo gumu kujua lini kinakuja, ila kwa yote tunasema JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

No comments: