Sunday, December 23, 2012

STORY ZA aSUBUHI HII KUTOKA MUSOMA , BUTIAMA

Story za Ahmad Nandonde, 

BUTIAMA

SERIKALI imetangaza kuwa haitasambaza Nishati ya umeme katika eneo ama kijiji ambacho wananchi wake watahitaji kulipwa fidia yoyote ikiwemo ya mazao mashambani.

Waziri wa Nishati na Madini Mh SOSPETER MUHONGO,ametangaza uamzi huo wakati akizungumza na wananchi wa vijiji Kuwaki,Kiriba,Bwai paris na Bwai londan katika wilaya ya Butiama mkoani Mara.

Amesema Serikali imedhamilia kwa dhati kusambaza nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini lakini kamwe haitaweza kufanya hivyo katika vijiji ambavyo vitakuwa na migogoro ya maeneo yatakayo hitajika kwaajili kupitishia njia umeme kwa madai ya kutaka fedia ama kushindwa kufyeka miti katika njia hizo.

Hata hivyo waziri huyo wa nishati na umeme ambaye yuko mkoani Mara kutembelea na kakagua miradi ambayo iko chini ya wizara yake ikiwa ni pamoja na kuzungumza na wadau wa nishati na umeme,amewataka wananchi hao kulinda miundo mbinu ya umeme zikiwemo Transfoma katika maeneo yao.

Amesema endapo kutatokea hujuma yoyote ya miundo mbinu ya umeme serikali kupitia Tanesco haitakuwa tayari kutumia gharama katika kurejesha nishati hiyo katika maeneo hayo.

MUSOMA

SIKU chache baada ya kutokea kwa mauji ya kinyama na kutisha katika wilaya za Butiama na Musoma mkoani Mara,Serikali imeombwa kuacha mdhaa na kuingiza siasa hivyo kusababisha kushindwa kuchukua hatua za haraka za haraka za kudhibiti ukatili huo ambao umesabisha hofu kubwa kwa wananchi.

Akizungumza waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka nchini Marekani,mbunge wa Musoma vijijini Mh Nimrod Mkono,ambaye yuko nchini humo kwa matibabu,amesema amesikitishwa na serikali kupitia jeshi la polisi kushindwa kuchukua hatua ambazo zitawezesha kukamatwa kwa watu wanahusika na unyama huo.

Amesema vitendo hivyo vya mauji ya kikatili,inawezekana vinahusisha watu wakubwa na wenye uwezo kifedha hivyo hatua ya jeshi la polisi kuendelea kukamata watu ili kujitoa katika dimbwi la lawama kutazidisha kuhimarisha zaidi mtandao huo na hivyo kutishia maisha ya wananchi wa maeneo hayo.

Pamoja na kutoa pole kwa wananchi wake kufuatia wimbi hilo la mauji hayo yanayoendelea jimboni kwake wilayani Butiama,mbunge huyo amelishauri jeshi la polisi kutumia kipimo cha vina saba DNA kwaajili ya kupambana na mtandao wa ukatili huo ambao umesababisha hofu kwa wananchi hata kushindwa kwenda mashambani kwa kuogopa kukamatwa na kuchinjwa.

Mbunge huyo wa Musoma vijijini amesema kama jeshi la polisi halina wataalam wa kufanya vipimo hivyo yuko tayari kuisaidia serikali kutafuta wataalam hao katika nchi ya Marekani na Uingereza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na unyama huo.

Tayari watu zaidi ya watatu wameuawa kwa kuchinjwa mithili ya kuku huku wauaji wakiondoka na viungo vyao vikiwemo vichwa ambapo zaidi ya watu kumi pia wameuawa kwa mapanga kwa nia hiyo hiyo ndani ya mwezi mmoja katika wilaya ya Butiama na Musoma mauji ambayo yamekuwa yakihusishwa na imani za kishirikina katika uchimbaji wa madini na uvuvi wa samaki.

No comments: