Sunday, December 23, 2012

JKT LATANGAZA VITA NA MAHARAMIA KANDA YA ZIWA

Story ya Ahmad Nandonde , BUNDA

JESHI la kujenga taifa JKT limetangaza kufa na kupona katika kupambana na vitendo vya Uharamia ambavyo vimekuwa vikisababisha mauji ya wavuvi,uporaji wa mali ukiwemo uvuvi haramu katika ziwa Victoria.
Mkuu wa kikosi cha JKT 822 KJ Rwamkoma mkoani Mara meja David Msakulo, ametangaza hali hiyo ya hatari kwa watu wanajihusisha na vitendo vya uharamia na uvuvi haramu katika ziwa victoria wilayani Bunda muda mfupi baada ya kuzinduliwa kwa kikosi cha uvuvi katika Mwalo wa Bulamba wilayani humo.
Amesema kikosi hicho teule cha Rwamkoma kitengo cha uvuvi kitafanya kazi kwa kushirikiana ma mamlaka za kiraia mbali na kutoa elimu ya kilimo,ufugaji na uvuvi kwa kutumia teknolojia za kisasa kwa wananchi pia kitatumika kupambana na vitendo hivyo vya uharamia na uvuvi haramu ambao umeshamili katika ziwa victoria na kutishia maisha ya wavuvi pamoja na kuchangia kupungua wingi wa samaki katika ziwa hilo.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe,akizungumza baada ya kufanya uzinduzi huo,amepongeza hatua ya jeshi hilo la kujenga taifa kukubali kuweka kikosi teule katika eneo hilo hatua ambayo itadhibiti vitendo viovu katika ziwa hilo vikiwemo vya uvuvi haramu jambo ambalo amesema litasaidia kuongeza idadi ya samaki kwa kipindi kifupi kijacho.

No comments: